![]() |
Rais wa TFF, Jamal Malinzi |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface
Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka
huu.
Aidha
aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo
hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati
ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki
na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa
majukumu yake.
Jamal
Malinzi
Rais
Dar
es SalaamNovemba 3, 2013
No comments:
Post a Comment