Sunday, December 28, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

LIGI KUU YA VODACOM YAINGIA RAUNDI YA 9

Wakati raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inakamilika leo (Desemba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu, ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano.

Coastal Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.

Ligi hiyo ambayo itachezwa mfululizo (non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani, itakamilisha raundi ya tisa Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji wa Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine.

Nayo mechi kati ya Mtibwa Sugar na Stand United ambayo jana ilivunjwa na mvua dakika ya 6 imemaliziwa leo ambapo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.

Wakati huo huo, mechi ya ligi iliyochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex imemalizika kwa wageni Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu. Bao hilo lilifungwa kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Hamisi Kasanga. 


MBAO FC YAKAMATA USUKANI SDL
Timu ya Mbao FC ya Mwanza imekamata uongozi wa Kundi B la michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya jana (Desemba 27 mwaka huu) kuizamisha JKT Rwamkoma ya Mara mabao 2-1.

Kwa matokeo hayo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao FC imeitoa kileleni JKT Rwamkoma baada ya kufikisha pointi tisa kwa kushinda mechi zote tatu dhidi ya Arusha FC, Pamba na JKT Rwamkoma. 

Mbao FC inafuatiwa na JKT Rwamkoma yenye pointi sita, Arusha FC pointi sita wakati Bulyanhulu na Pamba zikiwa za mwisho kwa pointi moja kila moja. Kundi hilo litakamilisha mzunguko wa kwanza Januari 3 mwakani kwa mechi kati ya JKT Rwamkoma na Arusha FC, na Bulyanhulu na Mbao FC.

Katika kundi A, Mji Mkuu (CDA) na Singida United ndizo zinazochuana kileleni kwa kufikisha pointi saba kila moja. Timu hizo zinafuatiwa na Milambo yenye pointi nne, Mvuvumwa FC yenye pointi moja wakati Ujenzi Rukwa ni ya mwisho ikiwa haina pointi.

Hata hivyo, Mvuvumwa FC na Milambo ziko nyuma kwa mechi moja. Mechi hiyo ya kukamilisha raundi ya tatu kati ya timu hizo itachezwa kesho (Desemba 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Kiluvya United imeendelea kuchachafya kundi C baada ya kushinda mechi zote ne ilizocheza, hivyo kufikisha pointi 12. Inafuatiwa na Mshikamano yenye pointi saba huku Abajalo ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 6.

Nafasi ya nne inashikwa na Transit Camp yenye pointi nne, Cosmopolitan yenye pointi mbili ni ya tano wakati Kariakoo ambayo haina pointi ni ya mwisho. Hata hivyo, Cosmopolitan na Kariakoo zina mchezo mmoja mkononi.

Mechi zinazofuata za kundi hilo ni Januari 3 mwakani kati ya Kariakoo na Mshikamano na Mshikamano (Ilulu), Transit Camp na Abajalo (Mabatini), na Cosmopolitan na Kiluvya (Karume).

Kundi D, vinara bado ni Njombe Mji yenye pointi 12 ikifuatiwa na Wenda yenye pointi sita wakati Volcano FC iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano. Mkamba Rangers ina pointi nne, Town Small Boys ina pointi moja wakati Magereza FC haina pointi.

Katika kundi hilo leo (Desemba 28 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys na Magereza itakayochezwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Januari 3 mwakani kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys na Njombe Mji, Volcano FC na Magereza, na Wenda na Mkamba Rangers.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayaya Mlele, mkoani Katavi wakifurahi jambo na Mama Tunu Pinda wakati alipofungua mkutano wao katika Shule ya Sekondari ya Mamba Desemba 28, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, December 8, 2014


Lowassa na askofu
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akimjulia hali Askofu Mkuu Katoliki Jimbo Kuu Tabora, Paul Ruzoka katika Hospitali ya TMJ Mikocheni Dar es Salaam leo. Picha na I.M.B.



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais aanza kazi rasmi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 8, 2010, ameanza kazi rasmi baada ya afya yake kuimarika kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita.
Mhe. Rais ameanza kazi rasmi kwa kumwapisha Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Daudi Felix Ntibenda katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais Kikwete katika moja ya majukumu ya kitaifa.
Kwa kuanzia Mhe. Rais atakuwa anafanya kazi za ofisini na kwa muda mchache. Muda na kasi ya kufanya kazi ya Mhe. Rais vitaongezeka kwa kadri afya yake inavyozidi kuimarika.
Na kwa sababu sasa ameanza kazi, Mhe. Rais ataanza kushughulikia mambo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake.
Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume katika Hospitali ya Johns Hopkins ya Baltimore, Maryland, Marekani Novemba 8, mwaka huu na alirejea nyumbani Novemba 29, mwaka huu.
Tokea awasili nyumbani, Mhe. Rais amekuwa anafanya mazoezi asubuhi na jioni kuimarisha afya yake kama alivyoshauriwa na madaktari.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
8 Desemba,2014

RAIS AANZA KAZI RASMI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais aanza kazi rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 8, 2010, ameanza kazi rasmi baada ya afya yake kuimarika kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita. Mhe. Rais ameanza kazi rasmi kwa kumwapisha Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Daudi Felix Ntibenda katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam. Kwa kuanzia Mhe. Rais atakuwa anafanya kazi za ofisini na kwa muda mchache. Muda na kasi ya kufanya kazi ya Mhe. Rais vitaongezeka kwa kadri afya yake inavyozidi kuimarika. Na kwa sababu sasa ameanza kazi, Mhe. Rais ataanza kushughulikia mambo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake. Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume katika Hospitali ya Johns Hopkins ya Baltimore, Maryland, Marekani Novemba 8, mwaka huu na alirejea nyumbani Novemba 29, mwaka huu. Tokea awasili nyumbani, Mhe. Rais amekuwa anafanya mazoezi asubuhi na jioni kuimarisha afya yake kama alivyoshauriwa na madaktari. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 8 Desemba,2014

Saturday, December 6, 2014

TAIFA STARS MABORESHO YAREJEA DAR

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu. Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Kenya Airways. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni. Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu. IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hotuba ya Sumaye Arusha leo

TAASISI YA UELIMISHAJI VIJANA WA SEKONDARI NA VYUO VIKUU HOTUBA YA MGENI RASMI MHE. FREDERICK T. SUMAYE WAKATI WA KUFUNGUA SEMINA ELEKEZI YA UHAMASISHAJI MAHALI: UKUMBI WA CCM MKOANI ARUSHA TAREHE: 06 DESEMBA, 2014 Ndugu ... Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Ndugu Nickson Mmanyi, Mwenyekiti wa Taasisi, Ndugu Hassan Joari, Katibu Mtendaji wa Taasisi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Baba Askofu, Ndugu zangu Wajumbe wa Mkutano, Ndugu Wanahabari, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana. Shukurani Napenda niwashukuru sana viongozi wa Taasisi hii ya kuwaelimisha vijana juu ya mambo mbali mbali kwa kunialika kuwa mgeni rasmi katika semina hii ya uhamasishaji wa vijana juu ya majukumu mbali mbali waliyonayo na yale yanayowapasa. Asanateni sana kwa heshima kubwa mliyonipa. Pili, napenda kuwapongeza sana viongozi kwa jinsi walivyosimamia shughuli kwa ufanisi mkubwa pamoja na mazingira magumu wanayokumbana nayo. Hongereni sana. Tatu, napenda kwa niaba ya viongozi wa Taasisi niwashukuru wote ambao kwa njia moja au nyingine wamewasaidia hawa vijana katika juhudi yao ya kufanikisha semina hii, na hao ni pamoja na Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha. Madhumuni ya semina Semina hii itashughulikia mambo matatu muhimu kwa vijana na kwa nchi yetu kwa ujumla. Mambo hayo ni pamoja na: · Nafasi ya vijana katika kulinda amani, usalama na utulivu wa nchi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 · Ujasirimali kwa vijana · Mikopo kwa wananfunzi wa vyuo vikuu na wa shule za sekondari. Hoja hizi zote ni muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu na maendeleo ya jamii kwa ujumla wake. Najua kuna mada zitakazotolewa juu ya hoja hizi na wataalam waliobobea lakini na mimi nigusie tu juu ya baadhi. Nafasi ya vijana katika kulinda amani, usalama na utulivu wa nchi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 1) Mambo yanayoathiri amani na utulivu Kwanza ili vijana hawa wawe walinzi wazuri wa amani, usalama na utulivu ni vema tukajikumbusha ni vitu au matendo gani yanayoweza kusababisha uvunjivu wa amani hasa wakati wa uchaguzi. · Siasa za chuki – ni vema vyama vya siasa vikaelewa kuwa nchi yetu iko katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, hivyo ni halali na haki kama kundi la watu wataanzisha chama cha siasa kwa kufuata taratibu na sheria inayohusika. Vyama vione kuwa kila moja ni mshindani wa mwenzake na siyo adui wa mwenzake. Ni nini basi nafasi ya vijana katika kusimamia jambo hili? Vijana ndiyo mara zote wanaotumika na vyama vya siasa ili kupambanisha na vijana wa chama au vyama vingine. Ni vema vijana mkaepuka hili la kutumika vibaya na vyama vya siasa na badala yake ninyi ndiyo mkawa wa kuzuia na kukemea vitendo vya aina hiyo. Fujo haijengi bali hubomoa misingi ya amani na utulivu wa nchi. · Vyama vya siasa na wafuasi wao kutotii sheria na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya mchakato mzima wa kampeni ikiwa ni pamoja na ratiba za kampeni na utaratibu mzima wa upigaji kura. Kuna vyama vya siasa ambavyo vikishagundua kuwa haviwezi kushinda basi huleta fujo katika katika mchakato wa kampeni nap engine huleta fujo hata kuwaumiza wafuasi wa chama kingine. Hapa napo vijana hutumika katika hujuma hizo zinazovunja amani na utulivu katika chaguzi zetu na nchi kwa ujumla. · Haki sawa kutokuonekana kutendeka kwa vyama vyote vya siasa. Hili ni jambo la hatari sana kwa amani na usalama wa nchi. Wakati wa uchaguzi ni lazima wahusika wote hasa tume ya uchaguzi lazima itende na ionekane inatenda haki sawa kwa kila mgombea wa kila chama. Upendeleo na uonevu wa aina yoyote iwe baina ya vyama au baina wagombea ni sumu kwa amani na utulivu wetu. · Kutokuwa na uwazi wa kutosha katika shughuli zote zihusuzo uchaguzi hasa wakati wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo. Hisia yoyote ya udanganyifu, upendeleo au uwizi wa kura ni sumu ya amani na utulivu. Uchaguzi ndipo mahali ambapo raia hutumia haki yake ya kuchagua na kuchaguliwa na hiyo haki yake ya msingi. Jambo lolote linalotafsiriwa kupokonya haki hii haitavumiliwa na hujibiwa kwa mapambano. Nchi nyingi hupoteza amani na utulivu wao katika hatua hii ya mchakato wa kura. · Kukataa matokeo. Nchi nyingi zimejikuta katika uvunjivu wa amani na utulivu kunapokuwa na chama au upande moja unaokataa matokeo ya kura zilizopigwa. Mifano ya hali hii ni mingi katika nchi za Afrika na mara kadhaa serikali zimeangushwa au kuishia katika mgawanyo wa madaraka jambo ambalo linawanyima raia haki ya kutetewa bungeni na upande wa upinzani ambao katika utaratibu huo nao huingia katika serikali ya mseto. Kuna wakati mwingine upande pinzani hukataa matokeo hata kama ni ya halali. Ni vema pale ambapo udhalimu haukutumika katika uchaguzi, vyama vyetu vikajua kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani na hakuna utaratibu ambao unawafanya washindani wote kuwa washindi. · Rushwa katika uchaguzi. Hili ni janga la demokrasia. Katika uchaguzi watu hutumia haki yao ya kuchagua kiongozi wamtakaye. Rushwa kama tujuavyo ni adui wa haki, kwa hiyo rushwa na uchaguzi wa haki haviwezi kuishi pamoja. Penye rushwa hakuna uchaguzi wa haki. Rushwa hapa ziko za aina kadha ambazo zote huathiri na kupoteza maana ya uchaguzi wa haki. Wako wanaotoa fedha ili kuwarubuni wapiga kura hivyo huwanunua wapiga kura kama bidhaa za sokoni. Mara nyingi watu hawa hutumia fedha nyingi sana ambazo hata hazijulikani zinatoka wapi na wakipata huo uongozi wanaoununua hizo fedha za watu zinarudije. Hawa mara nyingi wao wenyewe ni ama wala rushwa, ama wezi wa mali ya umma au wauza madawa ya kulevya. Vinginevyo hizo fedha nyingi namna hiyo wangezitoa wapi. Tatizo lingine linalofuatia mara baada ya hapo kama atakuwa amefanikiwa kuununua huo uongozi, basi kazi yake ya kipaumbele ni kuongeza kasi na viwango vya hiyo rushwa, uwizi wa mali umma au uuzaji wa madawa ya kulevya ili kurudisha fedha zake alizohonga nazo wapiga kura na faida kubwa juu yake. Hali hii huweka madarakani utawala mbovu na haki hutoweka kabisa katika nchi. Haki ikishatoweka haiwezekani kukawa na amani na utulivu. 2) Nafasi ya Vijana Vijana wana maslahi makubwa zaidi ya kuona kuwa nchi inakuwa katika hali nzuri ya maendeleo kuliko makundi mengine ya jamii. Hii ni kwa sababu vijana ndiyo wakaokaa katika nchi yao kwa muda mrefu zaidi hivyo ni lazima wapende kuishi katika nzuri ya baadaye. Vijana wanayo nafasi nzuri nay a wazi kutengeneza mazingira hayo ya kutengeneza nchi ya ndoto yao wakipenda. Lakini vijana pia wanayo nafasi ya kuiharibu nchi au kujitengenezea nchi ya hovyo ya baadaye. Vijana wanayo nafasi na uwezo wa kujijengea nchi nzuri watakayoipenda kwa kufanya mambo kadha ili nchi iwe na amani na utulivu, nitataja tu machache. · Kujenga uzalendo wa kweli kwa nchi yetu na kwa Watanzania. Inaonekana uzalendo unaanza kuwa bidhaa adimu katika nchi yetu. Vijana lazima muwe mstari wa mbele kulitambua hili na kusimamia maadili ya kujenga uzalendo wa kweli kwa watu wote. Kupoteza uzalendo ndiyo kunakosababisha watu kuwa waporaji wa mali umma bila huruma, kukosa uzalendo ndio kunakosababisha watu kula rushwa bila kujali kuwa kwa kufanya hivyo wanadhulumu haki za wengine, kukosa uzalendo ndiko kunakowafanya watu kufisadi mali ya uma bila kujali kuwa kwa kufanya hivyo nchi inaingia katika hasara kubwa na wananchi wanakosa huduma muhimu ambazo zingetengenezwa na mradi uliofisadiwa, kukosa uzalendo ndiko kunakosababisha watu kuwafanya watoto wa wenzao makontena yao ya kubebea madawa ya kulevya. · Kuweka madarakani serikali nzuri itakayosimamia maslahi ya umma na siyo maslahi binafsi. Tatizo kubwa sana katika nchi nyingi zinazoendelea hasa nchi za Afrika ni Uongozi Dhaifu na Utawala Mbovu. Kama hatutaweka madarakani viongozi wenye uzalendo wa kweli kwa nchi na watu wake, wenye uchungu na nchi na watu wake, na badala yake tukaweka wabinafsi, kama hatutaweka madarakani viongozi waadilifu na watenda haki na badala yake tukaweka wala rushwa au watoa rushwa, kama hatutaweka madarakani viongozi wachapa kazi na wenye dira ya kutuongoza watanzania na badala yake tukaweka wababaishaji; hatuwezikujenga nchi imara kiusalama na amani. · Kushiriki katika shughuli muhimu za uchaguzi. Huko nyuma tumekuwa na tatizo la vijana wengi kutokujiandisha kupiga kura na baada ya uchaguzi hubaki kulalamika kuwa viongozi waliopo siyo wazuri. Kama hukushiriki kuchagua kiongozi wako itabidi upokee waliyekuchagulia wenzako na wala usilalamike tena. Kama nilivyoeleza awali kuwa vijana lazima muweke madarakali serikali itakayowajibika kwa umma, huwezi kufanya hivyo kama hujajiandikisha kama mpiga kura. Kwa hiyo natoa wito kwa vijana wote wao wenyewe kujiandikisha kupiga kura na kwenda kupiga kura siku ya kupiga kura. Aidha vijana mnalo jukumu kubwa la kuwaelimisha umma nao kujiandisha kupiga kura na kwenda kupiga kura. Katika elimu hiyo ni muhimu wananchi wakaelimishwa madhara ya rushwa katika chaguzi zetu. Kura ni haki ya msingi sana ya mwanchi ambayo akiitumia vizuri atajiletea maendeleo na akiitumia vibaya kwa kuweka wala rushwa na mafisadi au wenye mapungufu mbali mbali, basi ajue amejinunulia au kujiwekea majanga ya maendeleo yake. · Kuwa mfano wa tabia njema katika jamii. Ili kudumisha amani na utulivu, vijana lazima wawe askari wema na watiifu wa jamii ambao wako tayari kupambana na maovu yote katika jamii yao. Vijana wasiwe askari wa kukodiwa au mamluki bali wawe askari waaminifu wa jamii. Vijana wawe ndiyo chachu ya maendeleo kwa sababu ndiyo nguvukazi ambayo jamii inaitegemea. Kwa ujumla vijana wakiwa washiriki wa mambo mema na wapinga mambo yote mabaya jamii itaishi katika amani na utulivu wa uhakika siyo nyakati za uchaguzi bali nyakati zote. Mwisho Kama tulivyoona vijana mnayo nafasi kubwa kuliko kundi lolote la kutengeneza nchi muitakayo kwa maisha yenu ya baadaye mkitumia karata zenu vizuri hasa wakati wa uchaguzi na fursa hiyo mnaweza kuitumia kwa kuanzia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Nawatakieni utekelezaji mwema wa haya yote na yote mtakayoelezana katika semina yenu elekezi. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
Mahafali ya nane ya Chuo cha Teknolojia DIT Jan 31, 2015 *Mahafali ya nane ya Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), yanatarajiwa kufanyika Januari 31, 2015 katika viwanja vya chuo hicho na yatatanguliwa na utoaji wa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wahitimu ambao wamefanya vizuri katika masomo yao.* *Taarifa ya DIT kwa vyombo vya habari imesema kuwa tuzo kwa wanafunzi zitatolewa Januari 23 mwaka huu ikiwa ni wiki moja kabla ya mahafali hayo ambayo wahitimu katika ngazi na masomo tofauti watatunukiwa.* *Wahitimu watakaotunukiwa ni siku hiyo ni pamoja na wa Stashahada ya Uhandisi (Ordinary Diploma), cheti cha awali cha TEHAMA (IT).

Thursday, December 4, 2014

SBL Yafungua Ghala Mbeya
 
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imefungua ghala lake kubwa la kwanza Mkoani Mbeya lenye uwezo wa kuhifadhi masanduku 80,000 mpaka 100,000 ya bia kwa ajili ya kuhifadhi na kusambaza bidhaa zake kwa wateja wake wote wa ndani na nje ya nchi.
 
Hayo ni mafanikio makubwa kwa SBL yaliyopatikana hivi karibuni katika nusu ya kwanza ya mwaka 2014. Ufunguzi wa ghala hilo utaleta mafanikio makubwa katika uendeshaji wa shughuli za SBL pamoja na kugusa maisha ya watu waliopo katika shughuri mbalimbali za uendeshaji wa SBL.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Bw. Steven Gannon alisema ghala hilo litaongeza uwezo wa kampuni kuzalisha bidhaa zake kwa wingi kwa wateja wake wa mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo ni Mbeya, Rukwa, Iringa na Ruvuma. Ghala hilo litasaidia kuweka akiba ya kutosha ya bia tofauti na hapo awali.
 
“Katika msimu huu wa Siku Kuu ya Krismasi na Mwisho wa Mwaka tunauhakika wa kukidhi mahitaji ya wateja wetu. Kila mtu atakunywa mpaka atakaporidhika na kwa ustaarabu,’’ alisema Bw. Gannon.
 
“Ufunguzi wa ghala hilI kwa kiasi kikubwa utapunguza gharama za usafirishaji kwa upande wa wasambazaji wetu  na kuongeza manunuzi zaidi. Hii itapunguza gharama zao za  muamala na hivyo kupata faida zaidi kwa kushirikiana na SBL,” aliongeza kusema Bw. Gannon.
 
Ufunguzi wa ghala hilo pia utatoa fursa zaidi za ajira katika nyanja mbalimbali za shughuli za SBL kama vile madereva, mafundi magari, mamalishe, makarani na kuongeza idadi ya wasambazaji.
“Matokeo ya mwisho ambayo ni muhimu zaidi kuliko yote kwa kufunguliwa ghala hili ni kuongezeka kwa mauzo kwa kampuni ya SBL, kwani wasambazaji zaidi kutoka nyanda za juu kusini watavutiwa kujiunga na biashara yetu kutokana na upatikaji huduma hiyo kwa urahisi,” alisema Bw. Gannon.
 
Mafanikio mengine ya SBL ni kwamba Novemba 23, 2014 walisherehekea kutimiza siku ya 1000 bila kupata ajali katika kiwanda cha SBL cha Mwanza, ambapo hiyo ni rekodi ya kwanza kuwekwa Tanzania na ya pili kwa Diageo.
 
Naye mgeni rasmi, Norman Sigalla alisema  ufunguzi huo ni hatua muhimu katika juhudi za kampuni ya SBL ya kuleta huduma zake karibu na wateja wake. Alisema hiyo ni hatua muhimu kwa watumiaji wa bidhaa hizo katika mikoa ya Nyanda za Juu kusini kwani sasa kutakuwa na upatikanaji wa uhakika na kwa muda wowote wa bidhaa za SBL.
 
Bw. Sigalla alisema Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini itanufaika na ufunguzi huo kwa sababu mawakala wa bidhaa za SBL walikuwa wanalazimika kwenda umbali mrefu kutafuta bidhaa hizo hivyo kuwaongezea gharama za uendeshaji. Jambo hilo lilipunguza sana soko la bidhaa za SBL katika maeneo hayo.
 
Mkuu wa Wilaya alisema kitendo hicho kilimnyima mteja/mnywaji haki yake ya msingi ya kuchagua kinywaji akipendacho, kwani alilazimika kunywa kile kinachopatikana kwa wakati huo.
 
Bw. Sigalla alisema Serikali inatambua mchango mkubwa utolewao na SBL kwa wakulima wa shayiri na mahindi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, akisema kwa kuingia nao mikataba ya kununua mazao yao wanafaidika kwa namna nyingi.
 
Alisema kipato cha uhakika wanachopata kutoka SBL kinawawezesha wakulima hao kumudu gharama mbalimbali za maisha kama vile kulipa karo za watoto wao wanaosoma, kulipia huduma za hospitali na mahitaji mengine muhimu.
 
Mkuu huyo wa Wilaya aliuomba uongozi wa SBL kufikiria kujenga kiwanda mkoani Mbeya ili kuongeza kasi ya ukuaji uchumi na kuongeza ajira kwa watu wenye sifa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
 

Youth in Tanzania: Start as young as you can in real estate business

Lamudi tream

     Lamudi Tanzania looks at the increase of young people investing in real estate in Tanzania
       
Buying rental properties becomes a popular option of investment for youngsters in recent years. The impressive 59.37 percentage of engagements among 25-34 men in Tanzania, according to a new survey from Lamudi, reveals that more and more people are willing to start as young as you can in real estate business.

The statistic research shows further that, compared with young people from 35-44 in the real estate business in the country, there is relatively higher engagement rate in th

“Youths are the ones to make changes in the industry” Country Manager of Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa commented on this phenomenon. However, there are definitely certain risks involved with investing rental properties in Tanzania, especially for young inexperienced investors.

“For a country to develop youth, we are supposed to be fully involved in the economic activities. There is a need to train the youth regarding the real estate business so as they can be conversant with the market. ” Godlove added.

As early as 2007, Tanzanian government issued the National Youth Policy. The mission is to improve the current sluggish supervision as well as to facilitate various youth economic development programs by participating in different sectors including real estate.
e 25-to-29 age group. Also 35% of house hunters and investors are youth from the same age group.
PRESS RELEASE
4/12/2014
MECHI YA NANI MTANI JEMBE KUCHEZWA TAREHE 13 DISEMBA
Mechi ya Nani Mtani Jembe 2 kati ya Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Disemba 13, 2014 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Udhamini wa TBL, George Kavishe amesema kwamba “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe 2 (Nani Mtani Jembe 2 Match). Pambano hili ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia saini makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni maalumu kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Alisema Nani Mtani Jembe 2 inahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga ambapo zawadi ya shilingi milioni 100 itatolewa na kugawanywa ifuatavyo.
  • Shilingi Milioni 20 ni zawadi ya mechi ya Nani Mtani Jembe ambapo timu itakayoshinda itapata sh milioni 15 na timu itakayofungwa itapata shilingi milioni 5.
  • Kampeni hii inaendeshwa kwa njia ya sms ambapo mashabiki wanapiga kura kwa njia ya sms na shilingi milioni 80 zimegawanywa kati ya timu hizo mbili ambapo kila timu ilianza na shillingi milioni 40 kwenye benki maalumu mtandaoni.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alisema mashabiki wa Simba na Yanga wanaweza kushiriki kwa kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager yenye ujazo wa mililita 500 ambapo mteja atabandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager na kuona namba maalumu. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo ambayo anatuma kwenda namba 15415 na kwa kufanya hivyo anakuwa amepunguza pesa taslimu shilingi 10,000 kutoka timu pinzani na kuichangia timu yake.
Kikuli pia alizikabidhi timu hizo jezi maalumu itakayovaliwa mahususi kwa ajili ya mechi hiyo na kuwahimiza mashabiki waendelee kuzipigia kura timu zao na kikubwa kuhakikisha wanafika uwanja wa taifa na kujionea wenyewe pambano hilo ambalo lazima mshindi apatikane.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura aliwakaribisha mashabiki na kuwaomba wajitokeze kwa wingi kwani hivi sasa timu hizo ziko kambini zikijiandaa na mtanage huo wa kukata na shoka unaotarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.
Alitaja viingilio vya mechi hiyo kuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP B, 20,000/= VIP C, 15,000/= kwa viti vya rangi ya chungwa kiingilio kitakuwa ni sh 15,000 huku viti vya bluu na kijani tiketi zikiuzwa kwa sh. 7,000/=.
Wambura alisema pambano hilo litakalosimamiwa na TFF litaanza saa kumi kamili na litachezwa kwa dakika 90 tu ambapo kama muda huo timu hizo hazitafungana basi mikwaju ya penati itapigwa ili mshindi apatikane.
Taji la Nani Mtani Jembe linashikiliwa na Simba ambao waliwafunga mahasimu wao 3-1 katika mechi iliyochezwa Disemba 21, 2013.
Mwisho.

 


Watanzania wana matarajio mengi kuhusu maisha yao ya baadaye
Wananchi wanamatumaini kuwa nchi itakuwa yenye uchumi wa kati ifikapo 2025

Mkurugenzi Twaweza, Rakesh Rajani
4 Desemba 2014, Dar es Salaam: Zaidi ya nusu ya wananchi (54%) wanafikiri kuwa maisha yao yatakuwa bora zaidi ifikapo mwaka 2025. Huu ndio mtazamo wa wananchi wakio katika makundi yote- vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake, na wakazi wa vijijini na mijini. Mtazamo huu ni tofauti kabisa na ule wa nchi za Marekani na Ulaya ambapo karibu wananchi saba kati ya kumi (65%) wanafikiri kuwa watoto wao watakuwa na hali mbaya zaidi kifedha kuliko walivyo wao sasa.
Matokeo haya yametolewa na Twaweza na Society for International Development (SID) kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Tanzania ifikapo mwaka 2025: Je, Watanzania wana matarajio gani na maisha yao ya baadaye? Muhtasari umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu za mkononi. Utafiti huu hufanyika katika maeneo yote Tanzania Bara (Zanzibar haimo kwenye matokeo haya). Matokeo haya yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,408 mwezi Agosti 2014.

Wakiangalia nchi kwa ujumla, wananchi wawili kati ya watatu wanaamini kuwa Tanzania itakuwa mahali pazuri pa kuishi mwaka 2025. Wananchi makundi yote bila kujali hali zao za kiuchumi wanaamini hivyo; mathalan, wananchi wenye kipato kikubwa 64% na wananchi maskini 68% wana matumaini na siku zijazo. Watanzania wana matumaini na akiba tuliyonayo kwa ajili ya nchi.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi bado wana wasiwasi. Karibu mwananchi mmoja kati ya watano (18%) wanahofia maisha yako yatakuwa mabaya zaidi mwaka 2025 kuliko yalivyo leo, na wapo wengine wanaodhani nchi itakuwa mahali pabaya pa kuishi mwaka 2025. Hapa kuna baadhi ya tofauti kati ya matajiri na maskini, mwananchi mmoja kati ya wanne katika kundi la matajiri (25%) na mmoja kati ya watano katika kundi la maskini (18%) hawana matumaini kuhusu siku zijazo.

Haijalishi mtazamo gani wananchi wanao, bado wanaamini kuwa matokeo na mustakabali wa Tanzania uko mikononi mwa Watanzania. Wananchi tisa kati ya kumi wanaamini kuwa viongozi wa Tanzania (54%) au wananchi (37%) watakuwa na udhibiti zaidi wa maamuzi ya nchi yao. Linapokuja suala la maisha yao wenyewe, wananchi wanaamini jitihada zao wenyewe kuwa ndizo zitazobadilisha maisha yao; wananchi sita kati ya kumi wanafikiri kuwa wao wenyewe ndio wenye ushawishi zaidi juu ya hatma yao ya baadaye. Hata hivyo, wakati mwananchi mmoja kati ya watano anaamini kuwa Serikali itakuwa na ushawishi mkubwa juu ya ustawi wa maisha yao ya baadaye, hakuna mwananchi wa mjini aliyetaja Serikali kama ina ushawishi muhimu. Mbali na wao wenyewe, wahojiwa wa mijini walitaja familia zao (20%) na marafiki au wenzao (19%) kuwa wenye ushawishi juu ya maisha yao ya baadaye.

Ukiangalia kila jambo moja baada ya jingine, karibu wananchi watatu kati ya wanne (72%) wanaamini kuwa Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025. Wananchi saba kati ya kumi (68%) pia wanafikiri kutakuwa na Rais mwanamke ifikapo mwaka 2025, na wananchi sita kati ya kumi (64%) wanatabiri kukua kwa uzalishaji wa viwanda na kupungua kwa kilimo. Kwa upande mwingine, wananchi wengi wanatabiri kutokea migogoro ya kidini (62%) na nusu yao (51%) wanatarajia kugawanyika kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chochote kitakachotokea huko mbeleni, wananchi wanaona mabadiliko makubwa, wananchi sita kati ya kumi wanatabiri kuwa upinzani utashinda urais, na tembo watapotea kabisa ifikapo 2025. Jambo la kushangaza, matukio mawili yenye uwezekano mdogo kutokea ni Tanzania kufuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia (38% ) na kuanzishwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki chini ya Rais mmoja (34%).

Mambo muhimu wanayotaka wananchi kwa siku zijazo ni maboresho kwenye huduma za kijamii (28% wanaona ni kipaumbele chao muhimu) na ukuaji wa uchumi (16% wanaona ni kipaumbele muhimu).

Aidan Eyakuze, Mkurugenzi wa shirika la Society for International Development, alitoa maoni yake kwenye matokeo haya "Watanzania kwa kiasi kikubwa wana matumaini na maisha yao binafsi ya baadaye, hasa ikilinganishwa na wenzao kutoka nchi zenye maendeleo makubwa kiuchumi, Marekani na Ulaya. Matumaini haya na mtazamo chanya ni mtaji mkubwa. Vinaimarisha uwezo wa nchi kusonga mbele kwa kujiamini na pia inaweka mzigo kwa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa tunafikia malengo ya mafanikio kwa nchi yetu."

Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema "Katika kipindi cha mabadiliko muhimu ya kitaifa na ya kimataifa, wananchi wa matabaka yote kiuchumi, maeneo na jinsia zote, wana matumaini kuhusu kile kilichopo siku za mbeleni nchini Tanzania. Changamoto kwa Serikali ya Tanzania, wasomi wa ndani pamoja na wananchi wenyewe, ni kuhakikisha kuwa matumaini haya yanaendelezwa kupitia utungaji sera na utekelezaji wenye ufanisi, kuhimiza maendeleo yenye usawa na kujenga mshikamano wa kijamii, ili matarajio ya wananchi ya maisha bora siku zijazo yafikiwe."