PRESS
RELEASE
4/12/2014
MECHI YA NANI
MTANI JEMBE KUCHEZWA TAREHE 13 DISEMBA
Mechi ya Nani
Mtani Jembe 2 kati ya Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager itachezwa Jumamosi, Disemba 13, 2014 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Udhamini wa TBL, George
Kavishe amesema kwamba “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza
mechi ya Nani Mtani Jembe 2 (Nani Mtani Jembe 2 Match). Pambano hili ni zawadi
ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia saini makubaliano kwamba
itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya
uhakika.”
Kavishe aliongeza
kuwa mechi hii ni maalumu kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe 2
ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu
hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium
Lager.
Alisema Nani Mtani
Jembe 2 inahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga ambapo zawadi ya
shilingi milioni 100 itatolewa na kugawanywa ifuatavyo.
- Shilingi Milioni 20 ni zawadi ya mechi ya Nani Mtani Jembe ambapo timu itakayoshinda itapata sh milioni 15 na timu itakayofungwa itapata shilingi milioni 5.
- Kampeni hii inaendeshwa kwa njia ya sms ambapo mashabiki wanapiga kura kwa njia ya sms na shilingi milioni 80 zimegawanywa kati ya timu hizo mbili ambapo kila timu ilianza na shillingi milioni 40 kwenye benki maalumu mtandaoni.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium
Lager, Pamela Kikuli alisema mashabiki wa Simba na Yanga wanaweza kushiriki kwa
kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager yenye ujazo wa mililita
500 ambapo mteja atabandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager
na kuona namba maalumu. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa
na namba hiyo ya kwenye kizibo ambayo anatuma kwenda namba 15415 na kwa kufanya
hivyo anakuwa amepunguza pesa taslimu shilingi 10,000 kutoka timu pinzani na
kuichangia timu yake.
Kikuli pia
alizikabidhi timu hizo jezi maalumu itakayovaliwa mahususi kwa ajili ya mechi
hiyo na kuwahimiza mashabiki waendelee kuzipigia kura timu zao na kikubwa
kuhakikisha wanafika uwanja wa taifa na kujionea wenyewe pambano hilo ambalo
lazima mshindi apatikane.
Mkurugenzi wa
Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura
aliwakaribisha mashabiki na kuwaomba wajitokeze kwa wingi kwani hivi sasa timu
hizo ziko kambini zikijiandaa na mtanage huo wa kukata na shoka unaotarajiwa
kuwa na msisimko mkubwa.
Alitaja viingilio
vya mechi hiyo kuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP B, 20,000/= VIP C, 15,000/= kwa
viti vya rangi ya chungwa kiingilio kitakuwa ni sh 15,000 huku viti vya bluu na
kijani tiketi zikiuzwa kwa sh. 7,000/=.
Wambura alisema
pambano hilo litakalosimamiwa na TFF litaanza saa kumi kamili na litachezwa kwa
dakika 90 tu ambapo kama muda huo timu hizo hazitafungana basi mikwaju ya penati
itapigwa ili mshindi apatikane.
Taji la Nani Mtani
Jembe linashikiliwa na Simba ambao waliwafunga mahasimu wao 3-1 katika mechi
iliyochezwa Disemba 21, 2013.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment