THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
aanza kazi rasmi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatatu, Desemba 8, 2010, ameanza kazi rasmi baada ya afya yake kuimarika
kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita.
Mhe.
Rais ameanza kazi rasmi kwa kumwapisha Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa
Daudi Felix Ntibenda katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam.
![]() |
Rais Kikwete katika moja ya majukumu ya kitaifa. |
Kwa
kuanzia Mhe. Rais atakuwa anafanya kazi za ofisini na kwa muda mchache. Muda na
kasi ya kufanya kazi ya Mhe. Rais vitaongezeka kwa kadri afya yake inavyozidi
kuimarika.
Na
kwa sababu sasa ameanza kazi, Mhe. Rais ataanza kushughulikia mambo yale ambayo
yamekuwa yanasubiri maamuzi yake.
Rais
Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume katika Hospitali ya Johns Hopkins ya
Baltimore, Maryland, Marekani Novemba 8, mwaka huu na alirejea nyumbani Novemba
29, mwaka huu.
Tokea
awasili nyumbani, Mhe. Rais amekuwa anafanya mazoezi asubuhi na jioni
kuimarisha afya yake kama alivyoshauriwa na madaktari.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
8
Desemba,2014
No comments:
Post a Comment