Monday, April 30, 2012

Ilivyo Ligi Kuu ya England kwa sasa


Wachezaji wa Man. United
WAKATI Ligi Kuu ya England ikifikia hatua za mwisho mwisho, mambo yanazidi kuziwia ngumu timu nne, ambazo zinatishiwa na kushuka daraja.
Mpaka sasa, Wolves inashikilia mkia wa ligi hiyo ikiwa na pointi 24 baada ya mechi 36 ikifuatiwa na Blackburn yenye pointi 31.
Timu za Bolton na QPR kila moja zina pointi 34 lakini QPR iko juu ya mstari wa timu tatu zinazotishiwa na kushuka daraja. Pamoja na kujipa matumaini hayo, Aston Villa na Wigan kila moja zina pointi 37 na zinaweza kushuka chini endapo tu Blackburn, Bolton na QPR zitashinda mechi zake na zenyewe kuharibu.
Wakati timu hizo zikishindana mkiani, Manchester City leo itakuwa nyumbani kuialika Manchester United huku kila upande ukijinasibu kushinda mchezo huo.
Makocha wa Pande zote, Roberto Mancini wa Manchester City na Alex Ferguson wa Man United wamekuwa na presha kila mmoja akitamani kushinda mchezo huo.
Mbali na mechi hiyo ya leo, mechi za mwishoni mwa wiki, Everton iliilaza 4-0 Fulham wakati Stoke ikiwa nyumbani, iliivimbia Arsenal na kutoka nayo sare ya 1-1 na Sunderland ilitoka 2-2 na Bolton.
 Swansea ilifungana 4-4 na Wolves huku West Brom na Aston Villa zikishindwa kufungana kabla ya Wigan kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Newcastle.
Chelsea iliikamua QPR mabao 6-1 na Tottenham iliilaza Blackburn mabao 2-0 katika mchezo mkali.

Africa Confederation Cup results


Mfungaji wa bao la tatu dhidi ya Shandi, Emmanuel Okwi 
27-29/04/12: Asec Mimosas (Ivory Coast) 1-1 CO Meknes
11-13/5/12: CO Meknes (Morocco) v Asec Mimosas
27-29/04/12: Warri Wolves (Nigeria) 3-1 Black Leopards
11-13/5/12: Black Leopards (South Africa) v Warri Wolves
27-29/04/12: Royal Leopards (Swaziland) 0-1 Club Africain
11-13/5/12: Club Africain (Tunisia) v Royal Leopards
27-29/04/12: Simba (Tanzania) 3-0 Al Ahly Shandy
11-13/5/12: Al Ahly Shandy (Sudan) v Simba
27-29/04/12: Heartland (Nigeria) 3-2 AC Leopards
11-13/5/12: AC Leopards (Congo Brazzaville) v Heartland
27-29/04/12: Enppi (Egypt) 3-1 CO Bamako
11-13/5/12: CO Bamako (Mali) v Enppi
27-29/04/12: Wydad Casablanca (Morocco) v AS Real de Bamako
11-13/5/12: AS Real de Bamako (Mali) v Wydad Casablanca (Morocco)
27-29/04/12: InterClube (Angola) 4-1 Al Amal Otbara
11-13/5/12: Al Amal Otbara (Sudan) v InterClube

Saturday, April 21, 2012

Chelsea yaitibulia Arsenal, zatoka suluhu Emirates

ARSENAL imeshindwa kutumia Uwanja wake wa nyumbani, Emirates baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Chelsea katika mechi ambayo walistahili ushindi kama siyo kupoteza nafasi za wazi za kufunga kulinganisha na wapinzani wao.
Vijana wa Chelsea walikuwa na sura mpya nane tofauti na kile kilichocheza kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Barcelona katikati ya wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Mbali na mchezo huo, matokeo mengine, Aston Villa imetoka suluhu na Sunderland wakati Blackburn iliilaza 2-0 Norwich.
Bolton na Swansea zilifungana bao 1-1 na Fulham ikaitandika 2-1 Wigan kabla ya
Newcastle kuirarua Stoke 3-0.
Dakika 45 za kwanza, Robin van Persie alikaribia kufunga kama siyo shuti lake kugonga mwamba, huku mpira wa kichwa wa Laurent Koscielny nao uligonga mwamba.
Van Persie alikosa nafasi zingine mbili nzuri za kufunga mwishoni mwa mchezo, huku Koscielny akicheza vizuri kuokoa hatari toka Daniel Sturridge.
Timu hizo zenye kawaida ya kucheza mechi yenye 'taaluma' ya kuvutia kila zinapokutana kwa miaka mingi,  mechi yao ya jana ilikosa mvuto na huenda ikasahaulika mapema.
Lakini itabaki kuwa changamoto kwa timu zote katika mbio za kusaka nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Arsenal inabaki nafasi ya tatu huku mechi tatu zikisalia, lakini Tottenham na Newcastle wako nyuma kwa pointi sita na michezo miwili mkononi.
Timu hizo mbili, ziko mbele ya Chelsea na mchezo mmoja mkononi ikiwa na maana kwamba, nafasi yao ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa itategemea wao kushinda taji hilo.

Wednesday, April 18, 2012

Congo organizes VCP for future stars
 A FIVB Grassroots Volleyball Cooperation Programme was held in Kinshasa, DR Congo from April 4 to April 7 with FIVB instructor Michel Vandermeulen of Belgium leading the course.
Thirty-seven participants learnt training methods and practice drills across the four-day event.
Shakob Woot, general secretary of the DR Congo Volleyball Federation was satisfied with the interest and the motivation shown from a new generation of players in the country, who proved that interest in the sport is not waning.
 

KAMATI YA NIDHAMU YATUPA RUFANI YA YANGA

Mechi iliyozua balaa kwa Yanga msimu huu.
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Aprili 17 mwaka huu) imetupa rufani ya Yanga iliyowasilishwa mbele yake kupinga uamuzi wa kupokwa pointi tatu kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili.
Aprili 2 mwaka huu Kamati ya Ligi ya TFF iliipa Coastal Union ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Yanga kumchezesha beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu hizo iliyofanyika Machi 31 mwaka huu wakati akiwa na adhabu ya kukosa mechi tatu.
Yanga katika rufani hiyo iliwasilisha sababu nane za kupinga kupokwa pointi hizo, kubwa zikiwa Cannavaro hakustahili kutumikia adhabu ya kukosa mechi tatu, si aliyempiga refa Israel Nkongo, ripoti za refa na kamishna wa mechi yao dhidi ya Azam zilionesha dalili ya njama (conspiracy) kwani zilifanana.
Pia Cannavaro alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao adhabu zao zilisimamishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Kamishna mstaafu wa Polisi, Alfred Tibaigana.
Katika uamuzi wake, Kamati imesema adhabu ya Cannavaro ya kukosa mechi tatu kwa mujibu wa Kanuni ya 25(c) ya Ligi Kuu ya Vodacom ilitolewa na refa na si Kamati ya Ligi kama ambavyo inalalamikiwa na Yanga, na kanuni hiyo haikatiwi rufani.
Pia barua ambayo TFF iliiandikia Yanga kuhusu adhabu ya mchezaji huyo ilikuwa wazi kwani ilikariri kanuni ya 25(c), hivyo kitendo cha klabu hiyo kumtumia mchezaji huyo ulikuwa ni uzembe wa kutoheshimu kanuni. Kama Yanga haikufahamu vizuri kanuni hiyo ilikuwa na fursa ya kuiandikia TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 25(f) ili kupata ufafanuzi kabla ya kuamua kumtumia mchezaji huyo.
Vilevile adhabu zilizokuwa zimesimamishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ni zile ambazo zilikuwa zimetolewa na Kamati ya Ligi, na si zile zilizotolewa uwanjani na refa.
Kuhusu madai ya conspiracy kwa ripoti za kamishna wa mchezo huo na refa, Kamati imebaini kuwa hazifanani, na suala lililokuwa likibishaniwa (contentious issue) lilikuwa ni kunyang’anywa pointi tatu.
Pia Kamati ilikariri Ibara ya 50 ya Kanuni za Nidhamu za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuwa mchezaji anayembughudhi refa kwa njia yoyote ile anastahili kufungiwa kwa angalau mechi sita.
 
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Saturday, April 7, 2012

Matokeo ya Ligi Kuu ya England leo

LONDON, England
Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wigan mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stanford Bridge kwa mabao ya Ivanovic na Diame waliofunga katika kila kipindi.
Kwa ushindi huo, matokeo hayo yanaifanya Chelsea kufikisha pointi 56
Nayo Sunderland ilitoshana nguvu na Tottenham wakati Bolton ikiwa nyumbani ilitandikwa mabao 3-0 na Fulham katika mchezo uliokuwa wa ushindani.
Mchezo mwingine uliikutanisha Liverpool inayochechemea kwa sare ya 1-1 na Aston Villa huku West Brom ikiibandua mabao 3-0 Blackburn, Norwich na Everton zenyewe zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2.

Tuesday, April 3, 2012

Barcelona, Bayern Munich nusu fainali Ulaya

Robinho akilimwa kadi.
BARCELONA na Bayern Munich zimetanguliwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufanya vizuri katika mechi zao za marudiano.
Katika mechi hizo, mabao mawili ya Lionel Messi na moja la Iniesta yameiwezesha timu hiyo kufikia hatua hiyo na kuifanya timu hiyo kufuzu kw ajumla ya mabao 3-1 dhidi ya AC Milan kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Washindi walipata bao la kwanza dakika ya 11 kwa mkwaju wa penalti uliofungwa  na Messi baada ya beki wa AC Milan, Luca Antonini kumwangusha ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru penalti na Messi hakufanya makosa..
Milan ilijibu dakika ya 31, Zlatan Ibrahimovic alipata mpira na kumpa pande, Antonio Nocerino ambaye naye alimlamba chenga, Javier Mascherano kabla ya kumtungua Victor Valdes ikiwa ni bao lake la 10 la msimu huu.
Katika dakika ya 41, Alessandro Nesta alimvuta jezi Sergio Busquets ndani ya eneo la hatari. Alionyeshwa kadi ya manjano na mwamuzi kabla ya Messi kuiingiza penalti kimiani penalti hiyo kuandika bao la pili.
Bao la tatu lilifungwa na Andres Iniesta aliyemalizia mpira uliopigwa na Messi na kumgonga, Philippe Mexes, kabla ya kumkuta Andres Iniesta ambaye naye hakufanya ajizi.
Kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Bayern Munich imefuzu kwa kuitoa Marseille ya Ufaransa kwa jumla ya mabao 4-0.
Ivica Olic alifunga mabao mawili, dakika ya 13 na 37 na kuifanya timu hiyo kusonga mbele katika nusu fainali. Mchezo wa kwanza ilishinda mabao 2-0.

Monday, April 2, 2012

Man United yalipa kisasi kwa Blackburn


Valencia baada ya kufumania nyavu
MABAO ya Antonio Valencia na Ashley Young yameiwezesha Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Blackburn na kuifanya timu hiyo kuwa mbele kwa pointi tano dhidi Man City.

Huku kila mmoja akiwa na mechi saba mkononi, United inaoyesha ni wazi imepania kutwaa taji la 20 msimu huu na Manchester City.

“Nina uzoefu na haya mambo, haijaslishi hata ukiwa mbele kwa pointi,” Ferguson alisema ambaye timu yake ililala mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Old Trafford.

Valencia aliambaa na mpira kutoka wingi ya kulia na kuachia shuti lililomshinda kipa Paul Robinson katika dakika ya 81. Young alifanya mambo dakika ya 86 kw akuandika bao la pili.
“Ilikuwa kazi kubwa. Tulipata upinzani mkali,” Ferguson alisema. “Kwa kipindi kiregu hatukutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Huu ni ushindi muhimu.”

Blackburn, sasa iko katika eneo la kushuka daraja huku kocha wake, Steve Kean ambaye tangu mwanzo alijaza viungo watano katikati  waliokuwa wakipandisha mfululizo mashambulizi.

MASHABIKI 11,056 WASHUHUDIA COASTAL, YANGA


Kikosi cha Yanga
MASHABIKI 11,056 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Coastal Union na Yanga lililochezwa (Machi 31 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Viingilio katika pambano hilo vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP, sh. 6,000 jukwaa kuu na sh. 4,000 mzunguko. Mapato yaliyopatikana kwenye pambano hilo ni sh. 61,494,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 14,664,927.80 uwanja sh. 4,630,335.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (DRFA) sh. 2,515,494.37.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 4,630,335.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,315,167.97 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 463,033.59.
Nayo mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa Machi 31 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 29,716,000 kutokana na watazamaji 8,167 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo.
Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni sh. 4,532,949.15, kila timu ilipata sh. 5,031,085.25, Uwanja sh. 1,486,465.08, TFF sh. 1,486,465.08, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,084,600.03, FDF sh. 743,232.54 na BMT sh. 148,646.51.
Wakati huo huo, pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Ruvu Stars lililochezwa Aprili Mosi Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam limeingiza sh. 1,585,000.
Jumla ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 1,000 mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu ni 1,569.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 283,656, uwanja sh. 57,942, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 117,306.08, TFF sh. 57,942, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 28,971 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 5,794.02.

TENGA AKATAA KUJIUZULU KWA MOHAMED

Leodegar Tenga
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amekataa barua ya kuomba kujiuzulu ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ya TFF, Said Mohamed.
Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa klabu ya Azam alimuandikia Rais Tenga barua ya kujiuzulu wadhifa huo akipinga kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Alfred Tibaigana juu ya adhabu zilizotolewa na Kamati ya Ligi kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga.
Rais Tenga amesema alimteua Mohamed katika Kamati hiyo kwa kuzingatia uadilifu wake na uwezo wake katika kuongoza, hivyo amekataa barua hiyo ya kuomba kujiuzulu.
Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Mkutano Mkuu wa TFF, Rais Tenga, Oktoba 28 mwaka jana aliunda Kamati ya Ligi ambayo wajumbe wake wanatoka kwenye klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza.
Wajumbe wa kamati hiyo ni Wallace Karia (Mwenyekiti), Said Mohamed (Makamu Mwenyekiti), Damas Ndumbaro, Steven Mnguto, Geoffrey Nyange, Seif Ahmed, Henry Kabera, ACP Ahmed Msangi, Meja Charles Mbuge na Ahmed Yahya.