Tuesday, April 3, 2012

Barcelona, Bayern Munich nusu fainali Ulaya

Robinho akilimwa kadi.
BARCELONA na Bayern Munich zimetanguliwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufanya vizuri katika mechi zao za marudiano.
Katika mechi hizo, mabao mawili ya Lionel Messi na moja la Iniesta yameiwezesha timu hiyo kufikia hatua hiyo na kuifanya timu hiyo kufuzu kw ajumla ya mabao 3-1 dhidi ya AC Milan kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Washindi walipata bao la kwanza dakika ya 11 kwa mkwaju wa penalti uliofungwa  na Messi baada ya beki wa AC Milan, Luca Antonini kumwangusha ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru penalti na Messi hakufanya makosa..
Milan ilijibu dakika ya 31, Zlatan Ibrahimovic alipata mpira na kumpa pande, Antonio Nocerino ambaye naye alimlamba chenga, Javier Mascherano kabla ya kumtungua Victor Valdes ikiwa ni bao lake la 10 la msimu huu.
Katika dakika ya 41, Alessandro Nesta alimvuta jezi Sergio Busquets ndani ya eneo la hatari. Alionyeshwa kadi ya manjano na mwamuzi kabla ya Messi kuiingiza penalti kimiani penalti hiyo kuandika bao la pili.
Bao la tatu lilifungwa na Andres Iniesta aliyemalizia mpira uliopigwa na Messi na kumgonga, Philippe Mexes, kabla ya kumkuta Andres Iniesta ambaye naye hakufanya ajizi.
Kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Bayern Munich imefuzu kwa kuitoa Marseille ya Ufaransa kwa jumla ya mabao 4-0.
Ivica Olic alifunga mabao mawili, dakika ya 13 na 37 na kuifanya timu hiyo kusonga mbele katika nusu fainali. Mchezo wa kwanza ilishinda mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment