![]() |
Valencia baada ya kufumania nyavu |
Huku kila mmoja akiwa na mechi saba mkononi, United inaoyesha ni wazi imepania kutwaa taji la 20 msimu huu na Manchester City.
“Nina uzoefu na haya mambo, haijaslishi hata ukiwa mbele kwa pointi,” Ferguson alisema ambaye timu yake ililala mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Old Trafford.
Valencia aliambaa na mpira kutoka wingi ya kulia na kuachia shuti lililomshinda kipa Paul Robinson katika dakika ya 81. Young alifanya mambo dakika ya 86 kw akuandika bao la pili.
“Ilikuwa kazi kubwa. Tulipata upinzani mkali,” Ferguson alisema. “Kwa kipindi kiregu hatukutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Huu ni ushindi muhimu.”
Blackburn, sasa iko katika eneo la kushuka daraja huku kocha wake, Steve Kean ambaye tangu mwanzo alijaza viungo watano katikati waliokuwa wakipandisha mfululizo mashambulizi.
No comments:
Post a Comment