
Vijana wa Chelsea walikuwa na sura mpya nane tofauti na kile kilichocheza kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Barcelona katikati ya wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Mbali na mchezo huo, matokeo mengine, Aston Villa imetoka suluhu na Sunderland wakati Blackburn iliilaza 2-0 Norwich.
Bolton na Swansea zilifungana bao 1-1 na Fulham ikaitandika 2-1 Wigan kabla ya
Newcastle kuirarua Stoke 3-0.
Dakika 45 za kwanza, Robin van Persie alikaribia kufunga kama siyo shuti lake kugonga mwamba, huku mpira wa kichwa wa Laurent Koscielny nao uligonga mwamba.
Van Persie alikosa nafasi zingine mbili nzuri za kufunga mwishoni mwa mchezo, huku Koscielny akicheza vizuri kuokoa hatari toka Daniel Sturridge.
Timu hizo zenye kawaida ya kucheza mechi yenye 'taaluma' ya kuvutia kila zinapokutana kwa miaka mingi, mechi yao ya jana ilikosa mvuto na huenda ikasahaulika mapema.
Lakini itabaki kuwa changamoto kwa timu zote katika mbio za kusaka nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Arsenal inabaki nafasi ya tatu huku mechi tatu zikisalia, lakini Tottenham na Newcastle wako nyuma kwa pointi sita na michezo miwili mkononi.
Timu hizo mbili, ziko mbele ya Chelsea na mchezo mmoja mkononi ikiwa na maana kwamba, nafasi yao ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa itategemea wao kushinda taji hilo.
No comments:
Post a Comment