Saturday, March 31, 2012

MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND LEO

Arsenal v QPR
ARSENAL imeshindwa kutamba mbele ya QPR baada ya kuchapwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya England na kuipunguza kasi ya timu hiyo kushinda mechi mfululizo.
Arsenal ambayo imezifunga timu mfululizo ikiwemo Tottenham na Newcastle, ilishindwa kabisa kuonyesha cheche mbele ya timu hiyo inayokabiliwa na balaa la kushuka daraja.
Alikuwa Samba Diakite aliyefunga bao la ushindi kwa timu yake.
Bao la kwanza la timu hiyo lilifungwa na Adel Taarabt baada ya kumpita Thomas Vermaelen kabla ya  Theo Walcott kuifungia Arsenal bao la kufutia machozi na lililokuwa la kusawazisha.
Nayo Chelsea iliibandua Aston Villa 4-2 na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 53 kwa mabao ya Daniel Sturridge na Branislav Ivanovic waliofunga mawili kila mmoja.
Mabao ya wenyeji yalifungwa na James Collins na Eric Lichaj.
Matokeo mengine, Wolves ikiwa nyumbani ilishindwa kutamba na kulazwa mabao 3-2 na Bolton wakati Everton ilishinda mabao 2-0 dhidi ya West Brom sawa na Wigan ilipoilaza Stoke mabao 2-0. Mchezo mwingine wa ligi hiyo, Fulham iliichapa 2-1 Norwich.
  

Tuesday, March 27, 2012

Heineken event speech by Koen Morshuis, General Manager, Heineken EA

Mheshimiwa waziri wa ofisi ya Raisi, Utawala Bora,

Ndugu Mathias Chikawe,

Wageni waalikwa,

Mabibi na mabwana.

Habari za jioni?

Ninayo furaha ya kuwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
On behalf of Heineken, I am delighted to be here with you this evening for
this very special occasion. Your presence here today demonstrates the
significant importance that you accord this special event, which pleases
and humbles us deeply. On behalf of the Heineken East Africa team, I thank
you for that.

Before we start on the actual reason for being here, please allow me to
share some highlights that make this occasion very special.

The UEFA Champions League is the most popular club football competition in
the world. UEFA created the UEFA Champions League back in 1992 from what
was previously known as the European Champions Clubs Cup, which dates back
to 1955. Twenty years later, it has a cumulative audience of 4.3 billion, a
global live audience of 1.1 billion, 55,000 hours of total coverage, 12,000
hours of live coverage, and distribution in 220 territories around the
world. The current Trophy has been an icon for many football fans since its
first introduction in 1967.

Its unique shape and size make it one of the most recognizable icons of the
UEFA Champions League, and the act of lifting it represents having won the
ultimate club football prize, therefore adding to its mystique and appeal
for both fans and players alike.

In May 2011, Heineken International announced that it had extended its
contract with UEFA to sponsor the UEFA Champions League for a further three
years. The 2011/12 season is the seventh consecutive year Heineken has
sponsored the prestigious UCL.

Heineken’s and UEFA’s main goal is to share the unique and memorable
experiences of the UEFA Champions League with fans all over the world, and
what better way than to be able to see the very prestigious Trophy itself
up close. Heineken is the biggest global premium beer brand, available in
almost every country in the world. Heineken originates from Amsterdam, the
Netherlands and therefore I am very delighted to have the Ambassador of the
Kingdom of the Netherlands, his Excellency Mr. Koekkoek with us at this
special moment in time, Your Excellency, thanks for being with us tonight.

As we like to say within Heineken “We were born in Amsterdam, but raised by
the world”. How great is it to be connected to the UEFA Champions League,
the biggest annual sporting event in the world !!

*The UEFA Champions League Tr**ophy Tour 2012 *presented by Heineken is a
true example of the globalization of both Heineken and the UEFA Champions
League where this year we touch ground with the actual Trophy in Mexico,
East Africa and China.

The choice of having the UEFA Champions League Trophy in Dar es Salaam at
this moment in time has of course a special reason. It s a fact that
Heineken has clearly recognized the potential of East Africa and therefore,
Heineken are currently setting up Operating Companies in Tanzania, Kenya
and Uganda. We are in the final stages of setting up our operations in
Tanzania and are recruiting a significant number of Tanzanians to support
our growth in the country.

We can say that we have experienced the warmth, ambition and dedication of
the Tanzanian people and feel welcome in your country, Asante Sana for
that….

I would also like to say a special Thank You to Mr and Mrs James
Rugemalira from
Mabibo Wines and Spirits and their team who have been the driving force
behind the success of Heineken in Tanzania over the last 17 years. We wish
you plenty of success on your renewed focus on the Windhoek and Xi brands
in Tanzania and are happy that you can share this special moment tonight
with us.

We are very excited to present the one and only UEFA CHAMPIONS LEAGUE
TROPHY. It is made of silver 925 on the outside, is gold plated on the
inside, and is engraved with the names of ALL the winners since 1956.

Now let us turn to the moment we have been waiting for: The official
unveiling of the UEFA CHAMPIONS LEAGUE TROPHY TOUR PRESENTED BY HEINEKEN.

Ndugu Mathias Chikawe, may I please invite you to come forward and
officially unveil THE ICON of the Champions of Champions……..
 
Thank You


VITA VPL YAHAMIA MORO UNITED, VILLA

Timu za Moro United na Villa Squad ambazo ziko kwenye vita ya kukwepa kushuka daraja katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinapambana Machi 28 kwenye moja kati ya mechi mbili za siku hiyo.
Mechi hiyo namba 153 itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili. Moro United iko nafasi ya 11 ikiwa na pointi 18 wakati Villa Squad iko nafasi ya 14 kwa pointi zake 14.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu. Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba akisaidiwa na Samson Kobe na Idd Mikongoti wote wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Arthur Mambeta wa Dar es Salaam wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Emmanuel Chaula kutoka mkoani Rukwa.
Mechi nyingine ya Machi 28 mwaka huu itakayochezeshwa na mwamuzi Judith Gamba wa Arusha itakuwa kati ya Ruvu Shooting itakayoikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Gamba katika mechi hiyo namba 150 atasaidiwa na Saada Tibabimale kutoka Mwanza na Hellen Mduma wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba ni Juma Safisha wa Pwani wakati Kamishna ni Hamis Kissiwa wa Dar es Salaam.
Mechi za Machi 31 mwaka huu ni Coastal Union dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi ya African Lyon na Simba.

Kombe la UEFA hadharani Tanzania

Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, UEFA
KOMBE la Ligi ya Mabingwa Ulaya, limewekwa hadharani kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinsky na kila mmoja alipiga nalo picha kama sehemu ya ukumbusho.
Mamia ya wageni waalikwa, walipiga nalo picha katika hafla iliyokuwa imechangamka na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Heineken ambao ndiyo wadhamini wakubwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kabla ya kufunuliwa hadharani na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangala, Kombe hilo lililokuwa linatokea Mexico na kutua nchini kupitia Kilimanjaro International Airport
Wakati Kombe lililokuwa limefunikwa kitambaa cheupe likifunuliwa, wimbo maarufu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ulikuwa ukipigwa na kupokewa kwa mashamsham huku fataki zikipigwa nje ya hoteli hiyo na kufanya anga za hoteli hiyo kupendeza.
Mapema, Mukangala aliwataka vijana wenye vipaji kujituma katika mazoezi waweze kusajiliwa na timu kubwa za Ulaya ili nao siku moja waweke historia kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Fenella aliyasema hayo juzi usiku kwenye Hoteli ya Kempinsky wakati wa kulionyesha Kombe la Ulaya (Ligi ya Mabingwa) hadharani.
Moja ya mechi za Ligi ya Mabingwa, Barca vs Panathinaikos
Alisema kuwa ujio wa kombe hilo si tu kwa ajili ya kulitazama, bali ni changamoto kwa vijana wacheze mpira, kujituma ili nao wapate nafasi ya kucheza soka Ulaya na kupata tiketi ya kucheza kombe hilo.
Dk. Fenella pia alitumia nafasi hiyo kuwataka Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kuandaa mashindano mengi yanayofanana na Uefa hasa kwa timu za vijana ili iwe changamoto kwao.
Mbali na hayo, aliwataka wadhamini wa michuano hiyo ya Uefa Kampuni ya Bia ya Heineken kuidhamini timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars kwani ni moja ya timu zinazopiga hatua katika maendeleo ya soka.
"Ningependa kuwashauri Heineken kujikita zaidi katika kudhamini soka Tanzania na hasa soka ya wanawake pamoja na kuidhamini Twiga Stars na pia kuangalia maendeleo ya soka kwa vijana.
"Sisi kama serikali tuitakuwa pamoja na tunataka kuona kunakuwepo na ustawi wa soka kwa vijana ambao ndiyo msingi wa maendeleo husika," alisema Fenella ambaye aliwashukuru waandaaji wa ziara hiyo kwa kukubali kulileta kombe Tanzania.
Kombe hilo lililotokea Mexico liliingia nchini Jumamosi iliyopita na linaondoka  Jumatano kwenda Kenya na baadaye kuendelea na ziada yake nchini China.
Meneja wa Heineken Afrika Mashariki, Koen Morshuis alisema kuwa Tanzania imeteuliwa kama nchi ya kwanza Afrika kufikiwa na kombe hilo kwa kuwa ina mashabiki wengi wanaofuatilia michuano ya Uefa ikifutiwa na Kenya.
mwisho

Monday, March 26, 2012

Manchester United yaipiga Fulham 1-0


MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amefunga bao la 29 la Ligi Kuu ya England lililoiwezesha Manchester United kuendelea kuongoza mbele ya mpinzani wake City kwa kufikisha pointi 73.

Rooney aliunganisha mpira wa Jonny Evans kwa kuukwamisha mpira wavuni mwa Fulham katika mechi hiyo iliyokuwa ya upinzani.

Ashley Young alikosa nafasi nyingi za wazi ambazo zingeisaidia United  kupata mabao zaidi lakini hata hivyo, kipa wa Fulham, Mark Schwarzer alikuwa kikwazo.
Hata hivyo, Fulham ilinyimwa openalti ya wazi baada ya Michael Carrick kumwangusha Danny Murphy ndani ya eneo la hatari lakini mwamuzi akapeta.

SAHIHISHO, LIGI KUU YA ENGLAND

 1 Man City 30 50 70
2 Man Utd 29 46 70
 3 Arsenal 30 22 58
 4 Tottenham 30 18 55
5 Chelsea 30 15 50
 6 Newcastle 30 2 50
7 Liverpool 30 5 42
 8 Sunderland 30 5 40
 9 Everton 30 -2 40
 10 Swansea 30 -2 39
 11 Norwich 30 -6 39
12 Stoke 30 -12 38
 13 Fulham 29 -3 36
14 West Brom 30 -5 36
15 Aston Villa 29 -7 33
16 Blackburn 30 -19 28
 17 Bolton 29 -25 26
 18 QPR 30 -20 25
19 Wigan 30 -28 25
20 Wolves 30 -34 22

Zawadi Copa Coca-Cola zawekwa hadharani

Moja ya mechi za Copa Coca-Cola mwaka jana
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola imeongeza zawadi za washindi wa michuano ya vijana ya Copa Coca-Cola kuanzia mwaka huu kutoka shilingi milioni 4.5 hadi  milioni 8 kwa timu itakayotwaa ubingwa. Coca-Cola, ambao ndio wadhamini wa michuano hiyo pia wameanzisha  zawadi ya shilingi laki nane kwa mwamuzi bora wa michuano hiyo ambayo itahusisha mikoa yote 28 ya Tanzania Bara na Visiwani.
Akiongea wakati wa semina elekezi ya Makatibu wakuu wa vyama vya mpira wa miguu nchini iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Coca-cola Kwanza Evans Mlelwa alitangaza zawadi ya mshindi wa pili kuwa ni shilingi milioni 4.8 wakati mshindi wa tatu atapata milioni 3.2.
Zawadi ya timu yenye nidhamu ni  shilingi milioni 1.6 badala ya  milioni moja za awali,  huku mchezaji bora, mfugaji bora na  mlinda mlango bora watazawadiwa shilingi laki nane kila mmoja badala ya laki tano za   ya awali kwa kila mmoja.
Huu ni mwaka wa sita mfululizo Coca-Cola kudhamini michuano hiyo ambayo huanzia ngazi ya wilaya mpaka Kitaifa ikiwa na lengo la kutafuta na kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu hapa nchini Tanzania. Mlelwa alisema kampuni ya Coca-Cola imejisatiti kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michezo ili kuleta maendeleo katika soka la Tanzania.
Semina elekezi hiyo iliwakutanisha pamoja Makatibu Wakuu wa Vyama vyote vya Soka nchini pamoja na watendaji wa soka la vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Mkurungenzi Mtendaji wa Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michezo, Leonard Thadeo, aliwapa changamoto makatibu wakuu hao kuhakikisha soka katika mikoa yao inapanda. ‘Fedha tunayopata kutoka Coca-Cola ni muhimu sana, tunatakiwa kuweka juhudi zetu hili kufanikisha ndoto zetu’, alisema Thadeo.
Usajili wa wachezaji wa Copa Coca-Cola unaendelea nchini nzima huku michuano ngazi ya wilaya ikitarajiwa kuanza Aprili mwaka huu na kumalizika Mei 5. Kulingana na TFF, mechi za Copa Coca-Cola ngazi ya Mkoa zitaanza kutimua vumbi kati ya  Mei 16 na Mei 25 huku michuano ya Kitaifa ikitarajiwa kufanyika kuanziaa  Juni hadi  Julai jijini katika miji ya  Dar es Salaam na Pwani.

Sunday, March 25, 2012

Wachezaji wa ES Setif wakiwa hawaamini kilichotokea
Samuel Sitta, Fedrick Sumaye, Said El Maamry na Zito Kabwe wakati wa mpambano wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba na ES Setif kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ilishinda mabao 2-0.
Saa chache kabla ya waarabu wa ES Setif kutandikwa mabao 2-0 na Simba.

Simba sasa yahitaji sare au ushindi Algeria

Simba wakishangilia bao la kwanza dhidi ya ES Setif
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba Sports Club, inahitaji sare ama ushindi iweze kuingia hatua ya makundi ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baadaye Aprili.
Simba iliilaza ES Setif ya Algeria katika mchezo mkali uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na mashabiki 41,050 licha ya mpambano huo kuonyeshwa live na Clouds TV.
Mabao ya Simba ambayo yamewekwa kimiani na Emmanuel Okwi na Haruna Moshi 'Boban' yataisaidia kwa kiasi kikubwa kuweka uhai kwa timu hiyo ambayo pia haitakiwi kwenda Algiers kwa kujiamini.
Ili kuitoa Simba, inatakiwa kuipiga mabao 3-0 kitu ambacho kwa timu za Waarabu kinawezekana. Kikubwa sasa Simba wajiandae kwa kila aina ya hila za waarabu kwani watafanya kila aina ya kile kinachowezekana kushinda mchezo huo.
Lakini Simba si timu ya kubahatisha, Simba si wageni wa waarabu na tunaamini wanatambua mbinu zao na wanatakiwa kujipanga mapema na wakitaka kuwamaliza ni kusaka bao la mapema.

Mukubwa kuzindua Utukufu wa Mungu Pasaka

Solomon Mukubwa
MWIMBAJI nguli kutoka Kenya, Solomon Mukubwa, anatarajia kuzindua albamu yake mpya ya nne ya Utukufu wa Mungu katika tamasha la muziki wa Injili la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, alisema Dar es Salaam jana kuwa Mukubwa ameahidi kufanya mambo makubwa atakapotumbuiza.

Msama alisema mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu mwenye ulemavu wa mkono mmoja, hivi sasa anatamba na albamu hiyo anayoamini itamng'arisha katika tamasha hilo.

Kabla ya Utukufu wa Mungu, Mukubwa amewahi kutamba na albamu ya Usikate Tamaa yenye nyimbo za Usikate Tamaa, Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri.

Mukubwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), anayeishi Kenya, pia amewahi kutoa albamu mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.

Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio.

Albamu yake ya pili ya Mungu Mwenye Nguvu ina nyimbo za Mungu Mwenye Nguvu, Mkono wa Bwana, Mfalme wa Amani, Siku Moja, Tabia Ina Dawa na Roho Yangu Ikuimbie.

Mbali na Mukubwa, wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Mwinjilisti Faraja Ntaboba, Ephraim Sekeleti, Maryanne Tutuma, kundi la Glorious Celebration na kwaya ya Kinondoni Revival.

Msama alisema baada ya waimbaji hao kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Daktari wa Villa Squad aaga dunia

ALIYEKUA Daktari mkuu wa timu ya soka ya Villa Squad Fc ‘Kambimoto’ Nassoro Mahmoud amefariki dunia alfajiri ya kuamkia jana alipokua amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu na kutarajiwa kuzikwa jioni ya leo kijijini kwake Mbwewe,Tanga.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa Villa, Andrew Chale alisema kua Dkt Nassoro alikua akisumbuliwa ugonjwa kwa muda mrefu ikiwemo kifua na kupewa mapumziko na timu yake takribani miezi miwili iliyopita mpaka alfajiri ya jana alipopatwa na umauti.
“Villa tumeupokea msiba huu mzito wa daktari wa timu ambaye alikua muhimiri kwa Villa ni majonzi makubwa kwa kipindi hichi tutaendelea kumuezi daima na kukumbuka mchango wake” Alisema Chale kwenye taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa Villa, Alhaji Ramadhan Uledi, alisema habari za kifo hicho kimemshtua sana kwani kimekuja wakati mgumu kwa timu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini kwenye msimamo wa ligi hivyo kuendelea kuwaumiza na majonzi makubwa.
Daktari Nassoro alikuwa akitambuliwa na shirikisho la soka TFF na chama cha madaktari wa michezo Tasma kwa nyadhifa yake hiyo ya Udaktari wa timu na alikua akishirikiana na madaktari wenzake wa timu nyingine ikiwemo kutoa ushahuri wa kitiba.
Mwisho

Saturday, March 24, 2012

MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI

Mtihani kwa kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji na mechi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Machi 31 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA).
Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya mtihani huo ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Sitta: Viongozi wabovu wameua michezo

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema viongozi wanaoingia madarakani kwa mgongo wa rushwa, kutumia miti shamba na wenye mlengo fulani, ndiyo walioifikisha michezo hapa ilipo.
Samuel Sitta
Sitta aliyasema hayo leo alipokuwa akizngumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali katika Bonanza la Waandishi wa habari, lililofanyika kwenye ufukwe wa Msasani na kuandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo, TASWA.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali na kuandamana na michezo, Sitta alisema Tanzania imekuwa nyuma katika kila mchezo na hiyo ni kutokana na kuwa na viongozi wasiokuwa na dira.
"Tuko nyuma sana, katika soka hali ni mbaya, riadha kidoogo, lakini ngumi, kikapu na mwaka jana nilikuwa mgeni rasmi pale Uwanja wa Ndani wa Taifa katika fainali, ikawa mbaya, haiwezekani Watanania mil45 tukose watu wenye vipaji.
"Haiwezekani vinchi vidogo kama Afrika ya Kati, Chad waibuke na kuonekana zinatisha kuliko sisi, sasa ninyi waandishi wapasheni, msiwe watu wa kutupaka mafuta.
"Wamulikeni viongozi wasiowajibika, hawa ndiyo hao walioingia kwa mipango na wameingia kwenye vyama vya michezo kwa kutarajia vitu fulani na ndiyo hao wanatumia rushwa, fedha na mambo mengine ali mradi waingie madarakani na matokeo yake michezo imepoteza mwelekeo.
"Tunachotaka ni kuona michezo inapiga hatua na zaidi kuwekeza katika michezo na kama kutakuwa na viongozi wabinafsi, kamwe michezo haiwezi kusonga mbele," alisema.
Awali, Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, aliomba serikali kwa kushirikiana na TFF kukubalia siku moja kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika.
"Tunafahamu kuwa ni ghali, kuna mambo mengi, lakini ikijipanga, Tanzania inaweza kuwa mwenyeji siku moja kwani fainali za Afrika zitasaidia kutangaza nchi na tunaweza kutumia fainali hizo kwa kutangaza utalii wetu," alisema Pinto.

Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Matokeo Ligi Kuu ya England leo

LONDON, EnglandARSENAL imeendelea kufanya kweli katika Ligi Kuu ya England baada ya kuibandua Aston Villa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Arsenal wakishangilia
Mabao ya Kieran Gibbs, Theo Walcott na Mikel Arteta yanaifanya Arsenal kufikisha pointi 61 mbele ya Man United na Man City zinazoongoza ligi hiyo. Man United ambayo kesho inacheza na Fulham ina pointi 70 wakati City iliyokuwa ugenini jana usiku ilikuwa inacheza na Stoke City.
Ushindi na uhakika wa kuendelea kushikilia nafasi ya tatu ulichangiwa pia na suluhu ya Chelsea dhidi ya Tottenham ambazo ziko nafasi ya nne na tano. Chelsea sasa ina pointi 56 wakati Totts wamefikisha pointi 55.
Nayo Liverpool ikiwa kwenye uwanja wake wa Anfield, imeendelea kuwa nyanya baada ya kutandikwa mabao 2-1 na Wigan katika mechi iliyokuwa ya ushindani.
 Shaun Maloney alikuwa wa kwanza kufunga kabla ya Luis Suarez kusawazisha dakika ya 46. Gary Caldwell alimaliza nguvu za Liverpool kwa kuandika bao la pili.
Bolton ilipata faraja ya kumkosa Fabrice Muamba kwa kuilaza 2-1 Blackburn sawa na Norwich ilivyoitungua Wolves huku Sunderland ikiizabua 3-1 QPR. Swansea iliyokuwa nyumbani ilifungwa mabao 2-0 na Everton.

Tuesday, March 20, 2012

Wachu: I choose volleyball over football and athletics

It was a crucial moment when the Kenyan National team setter Jane Wachu shifted to volleyball while she was involved before in other sports like football and Athletics but at that time she didn’t realize that she will be one of the pillars of the Kenyan volleyball National team years later and she will be the African champion at both club and national team levels.
Wachu (1) with her coleagues in training.
When Wachu was 8 she became famous for her sprinting ability while she was a student in the primary school. At that age she was much faster than her colleagues and that property attracted the physical education teachers to choose her in the Athletics team to run in the sprints events.
“The teachers thought I’m talent to run in 100 and 200 m races as well as the long and high jump and I was already training for these kinds of events for years later,” remembered Wachu while she was thinking about her sports career.
What was more confusing to her is being involved also in the football team of her school and through which she was chosen also for the selected team of her region. “When I have become 16 years old I had to choose between volleyball, football and athletics and it was the crucial moment when the two coaches of the national team David Lung’aho and Paul Bitok visited me at school to choose me for the first time in the Kenyan volleyball national team. I was very happy with this news but I was confused because they told me I have to leave the other sports and concentrate only on volleyball.” Wachu Commented.
She didn’t think for a long time because she already preferred volleyball than others and she feels that it will be her future sport.
“I took my decision in few minutes and even when the Athletics coach asked me to participate in a sprint race I told him that my career in this sport is over and I have to concentrate on my main sport volleyball. Really I’ve got a lot of benefit from Athletics and football; they gave me the flexibility and the speed that I used properly in volleyball.
She started her career as an attacker in her club then her coach advised her to shift to the setter’s position as it the best to use her Athletic abilities.
When she was only 18 she had become a standing player in the Kenyan volleyball national team. In 2006 she played to the Kenya Pipeline, the club having the record of winning the African Club Championship title.
“After graduation I had a job of officer at Kenya Prisons and I decided at that time to leave Pipeline to represent Prisons where I work. It wasn’t an easy decision because Pipeline was the biggest Kenyan club and also the best in Africa but I had to start a new challenge in Prisons team in 2007.
It was only a year later when prisons won the African Club Championship in Cairo in 2008 taking over the giants Al Ahly of Egypt and Mouloudia of Algeria.
Wachu led again her club to win the African Club Championship to consecutive times in Mauritius 2010 and Kenya 2011 raising their record to three cups in four years. The last two titles were impressive because they gave the Kenyan team the berth to represent Africa at the FIVB Club World Champs in Qatar.
“Again with the National team Wachu led Kenya to retain the gold medals of the 2011 African Nations Championship to improve her CV when she led the Kenyans also at the 2011 World Cup in Japan.
“Now I dream to represent my country at the World Grand Prix, it is a good chance to play a lot of matches at the world level. We are not less than any other team in the world but we had much difficult life style. We had for example to prepare for the big competitions outdoors because we don’t have a hall to train in. I had also to wake up daily at 5 am to start my work as prisons officer working for 12 hours before starting my training. Add to this I had to do my home requirements liking cooking and washing my clothes which is not the case I think for the European players.” She concluded.

VILLA, JKT KUHITIMISHA RAUNDI YA 21 MACHI 21


Villa Squad
Mzunguko wa 21 wa Ligi Kuu ya Vodacom unakamilika Machi 21 mwaka huu kwa mechi namba 147 kati ya Villa Squad na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Machi 24 mwaka huu kutakuwa na mechi ya ligi hiyo kati ya Moro United na African Lyon. Mechi hiyo namba 149 itafanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi za Machi 28 mwaka huu ni Ruvu Shooting Stars itakayocheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi wakati Moro United itakuwa mwenyeji wa Villa Squad katika mechi namba 153 itakayofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Wachezaji 25 waitwa kambini Twiga Stars

Twiga Stars mazoezini
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha wachezaji 25 kitakachoingia kambini Machi 25 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya program yake ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Ethiopia.
Wachezaji walioitwa kambini ni Amina Salum (Lord Baden Sekondari, Pwani), Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (New Generation, Zanzibar),
Esther Mayala (Street Girls, Mwanza), Evelyn Senkubo (Mburahati Queens), Fadhila Hamad (Uzuri Queens) na Fatuma Bashiri (Simba Queens).
Wengine ni Fatuma Gotagota (Mburahati Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens), Fatuma Mustafa (Sayari), Fatuma Omari (Sayari), Hanifa Idd (Uzuri Queens), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (JKT), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens) na Mwanaidi Khamis (Uzuri Queens).
Mwapewa Mtumwa (Temeke), Rukia Khamis (Sayari), Semeni Abeid (Tanzanite), Siajabu Hassan (Evergreen), Tatu Salum (Makongo Sekondari), Upendo Jeremiah (Pangani, Tanga), Veneranda Mbano (Tanzanite), Zena Khamis (Mburahati Queens) na Zena Said (Uzuri Queens).
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MASHABIKI, WACHEZAJI 35 ES SETIF KUWASILI MACHI 21

ES Setif wakipasha
Kikosi cha watu 35 cha timu ya ES Setif ya Algeria kinatarajiwa kuwasili nchini Machi 21  saa 12 alfajiri kwa ndege ya EgyptAir kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba itakayochezwa Machi 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara huo una wachezaji, benchi la ufundi, viongozi wa timu, kiongozi wa msafara kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Algeria (FAF) wakati watatu ni waandishi wa habari.
Wachezaji 20 katika msafara huo ni Mohamed Benhamou, Sofiane Bengorine, Riadh Benchadi, Smain Diss, Farouk Belkaid, Khaled Gourmi, Mourad Delhoum, Said Arroussi, Mokhtar Benmoussa, Tarek Berguiga, Mohamed Aoudi na Amir Karaoui.
Wengine ni Mohamed El Amine Tiouli, Racid Ferrahi, Youcef Ghezzali, Youssef Sofiane, Mokhtar Megueni, Rachid Nadji, Abderrahmane Hachoud na Akram Djahnit. Kocha wa timu hiyo ni Alain Norbert Geiger ambaye ni raia wa Uswisi.

TAARIFA YA FRAT KWA VYOMBO VYA HABARI 20/03/2012

VURUGU ZILIZOTOKEA KWENYE MCHEZO WA VODACOM PREMIER LEAGUE TAREHE 10/03/2012 KATI YA TIMU YA YANGA NA AZAM
Wachezaji wa Yanga wakimshambulia Israel Nkongo.
ITAKUMBUKWA YA KWAMBA KWENYE MCHEZO KATI YA TIMU YA YANGA NA AZAM MCHEZO WA VODACOM PREMIER LEAGUE TAREHE 10/03/2012 MWAMUZI WA MCHEZO HUO ISRAEL NKONGO ALIPIGWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WA TIMU YA YANGA KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA DAKIKA YA KUMI NA MOJA YAMCHEZO, BAADA YA MWAMUZI HUYO KUFANYA MAAMUZI SAHIHI YA KUMUONYESHA KADI YA PILI YA MANJANO NA KUFUATIWA NA KADI NYEKUNDU MCHEZAJI WA YANGA HARUNA NIYONZIMA.
BAADA YA KUONYESHWA KADI NYEKUNDU MCHEZAJI HUYO BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA HAWAKUKUBALIANA NA ADHABU HIYO NA KUANZISHA VURUGU KWA MWAMUZI ISRAEL NKONGO NA HATA KUDIRIKI KUMPIGA. KATIKA TUKIO HILO LA KUMPIGA MWAMUZI WACHEZAJI WENGINE WALIPEWA KADI NYEKUNDU NA KUISABABISHIA TIMU YAO KUENDELEA NA MCHEZO WAKIWA NA WACHEZAJI PUNGUFU.
KUTOKANA NA TUKIO HILO CHAMA CHAMA CHA WAAMUZI NCHINI FRAT KINALAANI KWA NGUVU ZOTE VITENDO VYA VURUGU VILIVYOFANYWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA KWA VILE VITENDO HIVYO SI VYA KIUANAMICHEZO HASA KATIKA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU, MCHEZO UNAOCHEZWA KWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA MASHINDANO HUSIKA, NA KUWATAKA WACHEZAJI WOTE NCHINI KUTOFANYA KAMA WALIVYOFANYA BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA, KWANI WACHEZAJI HAO WAMEIPAKA MATOPE TIMU YA YANGA KWANI VITENDO HIVYO SI SEHEMU YA HISTORIA BORA YA WACHEZAJI WA TIMU YA YANGA.
AIDHA, FRAT INATOA PONGEZI ZA DHATI KWA KAPTENI WA TIMU YA YANGA NA TIMU YA TAIFA SHADRAK MSAJIGWA KWA KUONYESHA UKOMAVU KAMA KAPTENI KWA KUWAZUIA WACHEZAJI WAKE KUTENDA YALE WALIYOKUWA WANAKUSUDIA KUYATENDA PIA KAPTENI HUYO AMENUKULIWA NA VYOMBO VYA HABARI AKIKEMEA VITENDO VILIVYOFANYWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WENZAKE.
PIA FRAT INAMPONGEZA KOCHA MKUU WA TIMU YA YANGA KOSTADIN PAPIC KWA KUKEMEA VITENDO VYA WACHEZAJI WAKE NA KUIKEMEA NIDHAMU MBOVU ILIYOONYESHWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WA TIMU YAKE.
PIA TUNAWAPONGEZA WACHEZAJI WOTE NA DAKTARI WA TIMU YA YANGA,AMBAO KWA NAMNA MOJA WALIJARIBU KWA NGUVU ZOTE KUWAZUIA WACHEZAJI WALIOKUWA NA HALI YA KUMPIGA MWAMUZI WA MCHEZO HUO.
VURUGU HIZO ZIMEKEMEWA NA VIONGOZI WA SERIKALI, RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI NA WALE WOTE WANAOPENDA MAENDELEO YA MCHEZO HUO HAPA NCHINI.
CHAMA CHETU KINAUNGA MKONO KWA DHATI KAULI ILIYOTOLEWA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI KWA KUKEMEA VITENDO AMBAVYO HAVIKUZI MAENDELEO YA SOKA HAPA NCHINI BALI VINADUMAZA NA KUTUWEKA KATIKA SURA MBAYA KWA WADAU MBALIMBALI WA MCHEZO WA SOKA IKIWA NI PAMOJA NA KUFANYIKA KWA UHARIBIFU WA MALI ZA SERIKALI NA WATU BINAFSI BILA SABABU ZA MSINGI ZA KUHALALISHA MATENDO HAYO.
VITENDO VYA WACHEZAJI HAO VILIWAHI KUTOKEA MIAKA YA AROBAINI NA SABA KATIKA LIGI NDOGO NA SI KWENYE LIGI KUU NCHINI. KWA HIYO WALE WOTE WALIOFANYA VITENDO HIVYO WANAWAJIBIKA KUWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA VITENDO VYAO AMBAVYO VIMETENGENEZA HISTORIA MBAYA KATIKA LIGI KUU HAPA NCHINI.
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU HAPA NCHINI LIMEWEKA KANUNI NA TARATIBU AMBAZO KAMA TIMU HAIKURIDHIKA NA YALE YANAYOJITOKEZA KWENYE MCHEZO, ZITATAKIWA KUZIFUATA ILI KUDAI HAKI ZAO NA SI VINGINEVYO.
NI IMANI YETU KWAMBA MAFUNZO TULIYOYAPATA KUTOKANA NA TUKIO HILO YATABAKI KUWA SEHEMU YA HISTORIA NA KUTORUDIWA TENA NA TIMU YOYOTE. TIMU YA YANGA NI MIONGONI MWA TIMU KUBWA HAPA NCHINI AMBAPO WACHEZAJI, VIONGOZI NA WAPENZI WAKE WANAPASHWA KUWA MFANO BORA WA KUIGWA NA HILO LINAWEZEKANA ENDAPO KUTAKUWA NA UTASHI WA DHATI WA KUJENGA TIMU BORA NA YENYE KUHESHIMIWA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA.
MCHEZAJI MWASIKA MMOJA KATI YA WACHEZAJI WALIOSHIRIKI KUMPIGA MWAMUZI AMENIPIGIA SIMU AKINIOMBA RADHI MIMI NA WAAMUZI WOTE KWA UJUMLA NA KUNIOMBA NIMSAIDIE KUMUOMBEA MSAMAHA KWA MWAMUZI WA MCHEZO HUO LAKINI HIYO HAITOSHI;NAMSHAURI MCHEZAJI HUYO AJITOKEZE HADHARANI ASIOMBE RADHI KWA SIRI KWANI WALIOATHIRIKA SIKU ILE SI NKONGO PEKE YAKE NI PAMOJA NA WATU WENGINE AMBAO WALIKUJA KUONA MCHEZO WA SOKA NA SI MASUMBWI, NAAMINI MWASIKA ANAJUTIA MAKOSA YAKE NA NI MUUNGWANA, ATAJITOKEZA KUOMBA RADHI HADHARANI ILI AWE SEHEMU YA JAMII INAYOPENDA MAMBO MEMA.
MWISHO NAOMBA VIONGOZI WA YANGA, WAPENZI NA WACHEZAJI,KWAMBA HUU SI WAKATI WA KULUMBANA KWA YALIYOTOKEA BALI NI WAKATI WA KUJISAHIHISHA ILI AIBU ILE ISITOKEE TENA; TUSIPOKEMEA YALE YALIYOJITOKEZA JANA KWENYE UWANJA WA TAIFA KESHO TUTAFANYA VILE VILE KWENYE NCHI ZA WATU, ITAKUWA NI AIBU KWA TAIFA NA SI YANGA PEKEE NA HIYO SI HULUKA YA WATANZANIA.
MICHEZO NI FURAHA, UPENDO, UNDUGU, MSHIKAMANO NA KUSHINDANA.
 
LESLIE L LIUNDA
KATIBU MKUU
FRAT TAIFA

MTIBWA SUGAR, SIMBA ZAINGIZA MIL 31/-

Mechi namba 146 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na Simba iliyochezwa Machi 18 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro imeingiza sh. 31,230,000.
Jumla ya watazamaji 10,410 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000. Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,763,898.31 kila timu ilipata sh. 6,508,230.51, uwanja sh. 2,169,410.17.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) sh. 867,764.07, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,169,410.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,084,705.08, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 216,941.02 na asilimia 10 ya gharama za mechi sh. 2,169,410.17.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi sh. 120,000 na tiketi sh. 2,480,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 728,700 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kilipata sh. 624,600.

MKUTANO MKUU TFF APRILI 21

Rais wa TFF, Leodegar Tenga.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike Machi 24 na 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam umesogezwa mbele hadi Aprili 21 na 22 mwaka huu.
Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Machi 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais Leodegar Tenga uliamua kusogeza mbele Mkutano Mkuu kutokana na mtiririko wa matukio ndani ya TFF katika kipindi hicho.
Ajenda katika Mkutano Mkuu huo wa kawaida wa TFF kufungua kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kuthibitisha muhtasari wa Mkutano Mkuu uliopita, yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita, hotuba ya Rais, kupokea taarifa za utekelezaji za wanachama na kupokea taarifa ya utekelezaji ya Kamati ya Utendaji.
Nyingine ni kupitisha taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka uliopita, kupitisha taarifa ya wakaguzi wa hesabu na hatua zilizochukuliwa, kupitisha bajeti ya mwaka 2012, kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya TFF, kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na Wanachama au Kamati ya Utendaji, mengineo na kufunga kikao.

Tuesday, March 13, 2012

Waliompiga mwamuzi Nkongo wafungiwa

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Dar es Salaam jana (Machi 12 mwaka huu) imetoa adhabu kwa klabu mbalimbali na wachezaji sita wakiwemo watano wa Yanga.
Haruna Niyonzima wa Yanga akilalamika baada ya kupata 'red'
Villa Squad imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi namba 122 dhidi ya Azam iliyochezwa Februari 15 mwaka huu Uwanja wa Chamazi.
Pia klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa uwanjani kwenye mechi namba 129 dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Februari 19 mwaka huu Uwanja wa Manungu. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 8(13) ya ligi hiyo.
Nayo Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi namba 132 dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu. Pia klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 25(d) baada ya kuoneshwa kadi kuanzia tano kwenye mechi hiyo.
Mchezaji Juma Mohamed wa Polisi Dodoma amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kuwashambulia watazamaji kwa chupa ya maji katika mchezo namba 114 kati ya timu yake na Villa Squad uliochezwa Februari 11 mwaka huu.
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga amefungiwa mechi sita za Ligi Kuu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumshambulia mwamuzi Israel Nkongo kwenye mechi hiyo namba 132.
Wachezaji wengine wa Yanga walioadhibiwa kutokana na mechi hiyo ni Nurdin Bakari amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000, Omega Seme amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000, Jerryson Tegete amefungiwa miezi sita na faini ya sh. 500,000.
Stephano Mwasika amefungiwa mwaka mmoja na faini ya sh. milioni moja kwa kumpiga mwamuzi Nkongo. Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu.
Kamati ya Ligi imempongeza nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na mshambuliaji wa timu hiyo Hamis Kiiza kwa kuwa mstari wa mbele kuzuia wenzao kumshambulia mwamuzi. Pia imempongeza kocha Kostadin Papic wa Yanga kwa kukemea vurugu zilizofanywa na wachezaji wake.
Pia Kamati ya Ligi imeiagiza Sekretarieti kutoa waraka kwa makamishna wote wa ligi juu ya utaratibu wa wageni rasmi wakati wa mechi za ligi.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

KITUO FAINALI LIGI DARAJA LA KWANZA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea kupokea maombi ya uenyeji wa kituo cha Fainali za Ligi Daraja la Kwanza iliyopangwa kuanza Machi 31 mwaka huu ikishirikisha timu tisa.
Mikoa kadhaa imeshawasilisha maombi ya uenyeji lakini hakuna ambao umekamilisha masharti ya kulipa sh. milioni 25 TFF ikiwa ni gharama za uendeshaji wa fainali hizo.
Baadhi ya mikoa ambayo imeshatuma maombi ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo ni Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ruvuma na Tabora. Kamati ya Ligi itatangaza kituo cha fainali hizo baada ya Machi 15 mwaka huu ambayo ni siku ya mwisho kupokea maombi na kutimiza masharti yaliyowekwa.
Timu zilizofuzu kucheza hatua ya fainali kutoka kundi A ni Polisi ya Dar es Salaam, Mgambo Shooting ya Tanga na Transit Camp ya Dar es Salaam. Kundi B ni Mbeya City Council, Mlale JKT ya Ruvuma na Tanzania Prisons ya Mbeya wakati kundi C ni Polisi ya Tabora, Polisi ya Morogoro na Rhino Rangers ya Tabora.

TEMEKE UTD, SMALL KIDS KUSHUSHANA MACHI 31

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Dar es Salaam jana (Machi 12 mwaka huu) imeamua timu za daraja la kwanza za Temeke United na Small Kids zicheze mechi Machi 31 mwaka huu mjini Dodoma ili kupata moja itakayoshuka daraja.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 4 ya Ligi Daraja la Kwanza timu tatu zitashuka daraja, moja kutoka katika kila kundi. Kwa vile AFC ya Arusha na Manyoni ya Singida kutoka kundi C tayari zimeshashuka, Kamati ya Ligi imeamua Temeke United na Small Kids zilizoshika nafasi ya mwisho katika makundi yao ya A na B zicheze mechi hiyo ili kupata moja itakayokamilisha idadi ya timu tatu za kushuka daraja.
Baada ya kumalizika hatua ya kwanza ya Ligi Daraja la Kwanza, timu tisa zimefanikiwa kucheza hatua ya fainali ya Tisa Bora na nyingine tano za Burkina Faso ya Morogoro, Morani ya Manyara, Polisi ya Iringa, Majimaji ya Songea na Green Warriors (94KJ) zimefanikiwa kubaki Ligi Daraja la Kwanza.

LIGI KUU VODACOM YAINGIA RAUNDI YA 21

Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya 21 kesho (Machi 14 mwaka huu) kwa mechi mbili ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuikabili African Lyon.
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni ni sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 15,000.
Mechi nyingine ya kesho itachezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo Simba watakuwa wageni wa timu ya Polisi Dodoma.
Yanga itarejea tena uwanjani Machi 17 mwaka huu kwa pambano dhidi ya wenyeji Villa Squad litakalofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati siku hiyo hiyo Coastal Union itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Machi 18 mwaka huu kutakuwa na mechi tatu ambapo Simba itakuwa ugenini Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar, Toto African itaikaribisha Polisi Dodoma jijini Mwanza wakati Azam na Ruvu Shooting Stars zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Chamazi.

Monday, March 12, 2012

PAMBANO LA AZAM, YANGA LAINGIZA MIL 72/-

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam lililochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 72,731,000.
Jumla ya watazamaji 19,339 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh. 15,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,303,932.20 kila timu ilipata sh. 14,726,592.20, uwanja sh. 4,908,864.07.
  Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,963,545.63, TFF sh. 4,908,864.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,454,432.03, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 490,886.41 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,908,864.07.
 
  Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. waamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, tiketi sh. 3,540,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
 
  Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata tena sh. 1,353,730 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 1,160,340.
 
Powered by Sorecson : Creation de site internetBoniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Rose Muhando kupeleka Utamu wa Yesu Pasaka

Rose Muhando
MALKIA wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando, naye atakuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la nyimbo za Injili litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Alex Msama, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, Muhando amethibitisha kushiriki tamasha hilo.

"Katika tamasha la Pasaka mwaka huu ndipo Rose Muhando atapata fursa ya kutambulisha albamu yake ya nne ya Utamu wa Yesu ambayo haijawahi kuzinduliwa tangu aikamilishe," alisema Msama.

Albamu ya Utamu wa Yesu inabeba nyimbo saba ambazo ni Utamu wa Yesu uliobeba jina la albamu hiyo, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawa Sawa.

Msama alisema pia Muhando ataimba pamoja na Anastazia Mukabwa wa Kenya aliyeshirikiana naye katika albamu ya Vua Kiatu, na baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

"Mpaka sasa tunaendelea na mazungumzo na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa Injili, lakini Muhando atakuwepo na Mukabwa atakuja na kundi la waimbaji wake," alisema Msama.

Albamu ya Vua Kiatu inabeba nyimbo nane ambazo ni Vua Kiatu uliobeba jina la albamu hiyo, Ee Mungu, Usiwe Manamba, Nzizilela, Nishike Mkono Bwana, Wanaokudharau na Mfalme.

Mbali na Mukabwa, wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho wa Dar es Salaam, kundi la Glorious Celebration na Atosha Kissava kutoka Iringa.

Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo baada ya kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita za Afrika ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya.