KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Jan Poulsen amesema hana mpango wa kuwaita washambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa kuwa hawana mchango wowote kwenye timu.
Hatua hiyo imekuja baada ya waandishi wa habari kuhoji sababu za Poulsen kumwacha Samatta na Ulimwengu. Kocha akasema; "Siwezi kumwita Samatta wala Ulimwengu, kazi yao kudribo mipira, wakielekezwa hivi wakifika ndani wanafanya vile.
"Hawataki kusikiliza maagizo ya kocha na wamekuwa wanafanya wanavyotaka," alisema Poulsen baada ya timu yake kulazimisha sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza kuwania kucheza Fainali za Afrika 2013. Timu hizo zitarudiano Juni.
Anasema, anamwamini sana Boko kwa asilimia kubwa kuliko mchezaji mwingine katika safu ya ushambuliaji kwa kuwa Boko anabadilika na kiwango chake kinapanda.
Kocha huyo ambaye alisusia mkutano wa waandishi wa habari anasema kuwa Tanzania haina mipango na kinachotakiwa ni kutengeneza wachezaji tangu mwanzo, lakini si kukimbilia wachezji wanaoibuka.
Matokeo mengine;
Madagascar 0-4 Cape Verde
Tanzania 1-1 Mozambique
Rwanda 0-0 Nigeria
Ethiopia 0-0 Benin
Burundi 2-1 Zimbabwe
Kenya 2-1 Togo
Chad 3-2 Malawi
Seychelles 0-4 DR Congo
Congo Brazzaville 3-1 Uganda
Liberia 1-0 Namibia
The Gambia 1-2 Algeria
Guinea Bissau 0-1 Cameroon
Sao Tome 2-1 Sierra Leone
Matokeo haya ni kwa mechi zilizokuwa zikipigwa katika viwanja mbalimbali
No comments:
Post a Comment