Saturday, March 10, 2012

Yanga yalambishwa koni Uwanja wa Taifa

Azam FC imefanya kweli baada ya kuisulubu Yanga mabao 3-1 katika mechi kali ya Ligi Kuu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kukalia kiti cha Ligi Kuu ya Vodacom inayoendelea.
Yanga iliyokuwa inahitaji ushindi, angalau kuisogelea Simba, imeshindwa kufanya hivyo huku Simba nayo ikipigwa kumbo na Wana lambalamba hadi nafasi ya pili.
Simba iliyokuwa ikiongoza kwa kuwa na pointi 40, imeshushwa hadi nafasi ya pili kwani Azam wamefikisha pointi 41. Simba ina nafasi ya kurejea kileleni leo itakapokwaana na Toto African kwani ushindi wa timu hiyo utaifanya ifikishe pointi 43.
Hata hivyo, Simba ina nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, kwani Toto imeonyesha udhaifu mkubwa katika mechi zake.
Katika mchezo wa jana, mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na John Boko aliyefungwa mawili na Kipre Bolou huku bao la Yanga likiwekwa kimiani na Kenneth Asamoah.

No comments:

Post a Comment