Thursday, March 1, 2012

Kaseja ataka mashabiki kuwapa 'shavu'



NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja  amewataka mashabiki wa Si8mba na hata Yanga kuwapa sapoti bila kujali tofauti zao kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika Jumapili.
 Simba itacheza na Kiyovu katika mechi ya marudiano baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1 uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamirambo, mjini Kigali..

Kaseja alisema pamoja na kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Kiyovu, wananchi wa nchi hiyo walionyesha uzalendo wa hali ya juu mno tofauti na walivyozoea hapa Tanzania.

"Pamoja na kwamba Kiyovu inaupinzani nchini Rwanda lakini mashabiki wa timu zote za nchi hiyo waliungana na kuwa kitu kimoja na kuishangilia timu yao mwanzo hadi mwisho wa mchezo.
 "Hali hii ni tofauti sana na kwetu Tanzania ambapo inapokuja timu ya nchi nyingine kucheza na Simba ama Yanga lazima itapata mashabiki wa kuipa sapoti tena kwa asilimia kubwa," alisema Kaseja.
Alisema umefika wakati watanzania waige uzalendo unaoonyeshwa na matifa mengine katika kuzipa sapoti timu zao ili ziweze kufanya vizuri na kusonga mbele.

"Hii inachangia matoeo mabaya kwa timu za hapa nyumbani kwani mashabiki ni mchezaji wa 12 hivyo wanapokuja kucheza kwetu wanapata sapoti vivyo hivyo wanapokuwa kwao tofauti na sisi tunapotoka nje ya mipaka ya Tanzania hatupewi sapoti hiyo," alisema.

No comments:

Post a Comment