![]() |
Arsenal v QPR |
Arsenal ambayo imezifunga timu mfululizo ikiwemo Tottenham na Newcastle, ilishindwa kabisa kuonyesha cheche mbele ya timu hiyo inayokabiliwa na balaa la kushuka daraja.
Alikuwa Samba Diakite aliyefunga bao la ushindi kwa timu yake.
Bao la kwanza la timu hiyo lilifungwa na Adel Taarabt baada ya kumpita Thomas Vermaelen kabla ya Theo Walcott kuifungia Arsenal bao la kufutia machozi na lililokuwa la kusawazisha.
Nayo Chelsea iliibandua Aston Villa 4-2 na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 53 kwa mabao ya Daniel Sturridge na Branislav Ivanovic waliofunga mawili kila mmoja.
Mabao ya wenyeji yalifungwa na James Collins na Eric Lichaj.
Matokeo mengine, Wolves ikiwa nyumbani ilishindwa kutamba na kulazwa mabao 3-2 na Bolton wakati Everton ilishinda mabao 2-0 dhidi ya West Brom sawa na Wigan ilipoilaza Stoke mabao 2-0. Mchezo mwingine wa ligi hiyo, Fulham iliichapa 2-1 Norwich.
No comments:
Post a Comment