
Tanzania ni miongoni mwa mataifa 100 yatakayoshiriki Olimpiki itakayofunguliwa Julai 27 kwenye Uwanja maalumu uliopo London, Uingereza.
Katika michezo hiyo,Samson Ramadhani atakuwa akipeperusha bendera ya Tanzania katika mbio za Marathon (km 42) na mita 5,000 kwa Zakhia.
Wanariadha hao kwa nyakati tofauti walisema pamoja na kukabiliwa na mazingira magumu katika mazoezi yao lakini wanamatumaini ya kufanya vizuri kwenye michezo hiyo.
"Natambua ushindani tunaopata kimataifa, hali hiyo imenipa changamoto ya kufanya mazoezi zaidi nikabiliane na upinzani huo katika Olimpiki," alisema Zakhia.
No comments:
Post a Comment