Alisema ukiachia wachezaji waliondooka kipindi chao wachezaji walioko sasa kwenye timu yac Taifa wana muda mrefu bila kuleta maendeleo ya kweli kwa kuwa timu zina udhamini hivyo hakuna sababu ya kucheza bila uzalendo.
"Wachezaji wanacheza kama kujifurahisha au kuona ufahari kwamba wameshiriki kwenye michuano fulani,na wana ratiba wanajua kabisa kwamba koch akiita wachezaji ataniita tu lazima kwa kuwa ni wale wale kila siku hawabadiliki,na wanachofanya hakuna," alisema Matola.
Aliongeza kuwa ilitimu ipande badala ya kushuka ni vema wahusika wakaangalia tatizo ambalo kwa ktazamo wake ni kuwatumia wachezaji wakongwe kila siku bila kuwaandaa vijana ambao wataokoa jahazi siku zijazo au hizi ambazo timu imekuwa ikifanya vibaya.
No comments:
Post a Comment