Mwamuzi, Israel Nkongo akiwakwepa wachezjai wa Yanga |
Baadhi ya wachezaji, Stephano Mwasika, Nurdin Bakari na Nadir Haroub 'Cannavaro' walipandisha mzuka na kumpiga mwamuzi ambaye aliishia kumpa kadi nyekundu Cannavaro. Katika mchezo huo Yanga ilitandikwa mabao 3-1.
Huo ni mchezo wa tatu kwa Yanga kupoteza na kuichan Simba ikiwa imepoteza mechi chache, kati ya timu zinazoshiriki ligi hiyo.
Songombingo liianza baada ya Haruna Niyonzima kupewa kadi nyekundu baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi huyo. Awali alikuwa amepata kadi ya manjano kutokana na mchezo mbaya.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura alipoulizwa juu ya sakata hilo, alikataa kuzungumzia akisema TFF itakaa kuangalia nini cha kufanya.
Ukiacha hali hiyo, ilibidi polisi kutumia gesi z akutoa machozi kutawanya mashabiki waliokuwa wamejipanga nje ya uwanja wakidai wanamsubiri mwamuzi. Polisi walitumia gari la maji ya kuwasha na maeneo mengine walitumia gesi ya kutoa machozi na walifanikiwa kuwatawanya.
No comments:
Post a Comment