Moja ya mechi za Copa Coca-Cola mwaka jana |
Akiongea wakati wa semina elekezi ya Makatibu wakuu wa vyama vya mpira wa miguu nchini iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Coca-cola Kwanza Evans Mlelwa alitangaza zawadi ya mshindi wa pili kuwa ni shilingi milioni 4.8 wakati mshindi wa tatu atapata milioni 3.2.
Zawadi ya timu yenye nidhamu ni shilingi milioni 1.6 badala ya milioni moja za awali, huku mchezaji bora, mfugaji bora na mlinda mlango bora watazawadiwa shilingi laki nane kila mmoja badala ya laki tano za ya awali kwa kila mmoja.
Huu ni mwaka wa sita mfululizo Coca-Cola kudhamini michuano hiyo ambayo huanzia ngazi ya wilaya mpaka Kitaifa ikiwa na lengo la kutafuta na kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu hapa nchini Tanzania. Mlelwa alisema kampuni ya Coca-Cola imejisatiti kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michezo ili kuleta maendeleo katika soka la Tanzania.
Semina elekezi hiyo iliwakutanisha pamoja Makatibu Wakuu wa Vyama vyote vya Soka nchini pamoja na watendaji wa soka la vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Mkurungenzi Mtendaji wa Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michezo, Leonard Thadeo, aliwapa changamoto makatibu wakuu hao kuhakikisha soka katika mikoa yao inapanda. ‘Fedha tunayopata kutoka Coca-Cola ni muhimu sana, tunatakiwa kuweka juhudi zetu hili kufanikisha ndoto zetu’, alisema Thadeo.
Usajili wa wachezaji wa Copa Coca-Cola unaendelea nchini nzima huku michuano ngazi ya wilaya ikitarajiwa kuanza Aprili mwaka huu na kumalizika Mei 5. Kulingana na TFF, mechi za Copa Coca-Cola ngazi ya Mkoa zitaanza kutimua vumbi kati ya Mei 16 na Mei 25 huku michuano ya Kitaifa ikitarajiwa kufanyika kuanziaa Juni hadi Julai jijini katika miji ya Dar es Salaam na Pwani.
No comments:
Post a Comment