Saturday, February 25, 2012

Msumbiji 'The Mambas' kuwavaa Taifa Stars

Timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) itawasili nchini Jumapili Februari 26 kwa ndege ya South African Airways. Ndege hiyo yenye mruko namba SA 186 inatarajia kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.55 mchana.
  Msafara wa Mambas kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano (Februari 29 mwaka huu) saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa na watu 29. Kati ya hao, 19 ni wachezaji wakati waliobaki ni maofisa wa timu hiyo.
  Mwamuzi wa mechi hiyo Farouk Mohamed na wasaidizi wake Ayman Degaish, B.T Abo El Sadat na Gihed Greisha kutoka Misri watawasili nchini kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa ndege ya Egypt Air. Kamishna ni Loed Mc Ian kutoka Afrika Kusini.
  Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa Jumanne (Februari 28 mwaka huu) katika vituo vya vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha mafuta cha Bigbon kilichopo Msimbazi (Kariakoo), mgahawa wa Steers ulioko Barabara ya Samora/Ohio, Kituo cha mafuta cha Oilcom Ubungo na Uwanja wa Taifa.

YANGA WATAKIWA 40 TU UWANJANI CAIRO

Msafara wa Yanga utakaokuwa uwanjani kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek itakayochezwa wikiendi ijayo nchini Misri unatakiwa kuwa na watu wasiozidi 40.
Kwa mujibu wa maelekezo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) yaliyotumwa jana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ni idadi hiyo tu inayotakiwa kwa vile Zamalek inakabiliwa na adhabu ya kucheza mechi hiyo bila washabiki.
Adhabu ya Zamalek kutocheza mechi mbili za nyumbani za michuano hiyo bila washabiki ilitolewa Aprili 20 mwaka jana na Bodi ya Nidhamu ya CAF iliyokutana jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mechi dhidi ya Yanga ndiyo itakayokuwa ya kwanza kwa Zamalek kuanza kutumikia adhabu hiyo iliyotakana na washabiki wake kufanya fujo kwenye mechi ya michuano hiyo mwaka jana ilipocheza dhidi ya Club Africain ya Tunisia.
Hivyo kila timu (Yanga na Zamalek) katika mechi hiyo inatakiwa kuwa na wachezaji ambao wana leseni za CAF kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa 2012. Pia benchi la ufundi katika kila timu linatakiwa kuwa na watu watano.
Kwa klabu zote mbili, kila moja imeruhusiwa kuingia na wajumbe wake wa Kamati ya Utendaji wasiozidi kumi. Mbali ya klabu hizo mbili, wengine waliotajwa kuruhusiwa kuingia uwanjani ni vijana 20 watakaofanya kazi ya kuokota mipira (ball-boys).
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco ambao ni Jihed Redouane, Rouani Bouazza na Bekkali Mimoun wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Gihed Greisha wa Misri. Kamishna wa mchezo huo ni Ben Khadiga wa Tunisia.

Mashindano ya netiboli daraja la pili yafunguliwa Dar


Michuano ya netiboli Ligi Daraja la pili mkoa wa Dar es Salaam yamefunguliwa kwenye viwanja vya klabu ya Sigara jijini Dar es Salaam na Mama Tunu Pinda.
Timu mbalimbali zinashiriki mashindano hayo ambayo lengo hasa ni kusaidia kuinua mchezo huo na pia kupata timu za daraja la kwanza.

Upendo Nkone kupamba tamasha la Pasaka

MWANAMUZIKI wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Nkone anatarajiwa kuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mratibu wa tamasha hilo, Alex Msama wa Kampuni ya Msama Promotions, alisema Dar es Salaam jana kuwa Nkone amekuwa mwimbaji wa pili kuthibitisha kushiriki tamasha hilo baada ya Upendo Kilahiro.

Msama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, alisema anaamini tamasha la mwaka huu litakuwa bora zaidi kwa vile litashirikisha waimbaji wengi wakali.

Tamasha hilo la aina yake, baada ya kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

Tamasha la Pasaka mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Msama alisema tamasha hilo pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nkone alisema anaendelea vyema na maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo, na akatoa mwito kwa mashabiki wake wasiwe na wasiwasi, watarajie kupata mambo mazuri zaidi.

Aliwaomba mashabiki wamiminike kwa wingi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Aprili 8 na Jamhuri Aprili 9, kuona mambo mazuri aliyowaandalia.

Wachezaji Simba wajifua kwa nguvu

 Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi kwenye gym ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya Kiyovu ya Rwanda. Kocha wa timu hiyo, Cirkovic amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wachezaji wa timu hiyo kuzingatia mazoezi.

Chelsea yazidi kupasua anga England

CHELSEA imeibandua Bolton mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya England. Alikuwa, Mbrazil, David Luiz aliyefunga bao la kuongoza kwa timu hiyo kabla ya mshambuliaji wa Ivory Coast, Didier Drogba kufunga. Frank Lampard alifunga bao la tatu kwa kumalizia krosi ya Juan Mata.
Mechi nyingine za leo, West Brom iliyokuwa nyumbani iliitandika Sunderland mabao 4-0.
Nayo QPR ilishindwa kutumia uwanja wa nyumbani na kuchapwa bao 1-0 na Fulham wakati Newcastle ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 2-2 na Wolves. Wigan na Aston Villa zilitoka suluhu.
Drogba

Thursday, February 23, 2012

Upendo Kilahiro kupanda jukwaani Tamasha la Pasaka

Upendo Kilahiro
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili mwenye sauti nyororo,
Upendo Kilahiro amekuwa wa kwanza kuthibitisha kushiriki
katika tamasha la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka
 Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex

 Msama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama
Promotions, alisema Dar es Salaam kuwa Kilahiro
amemthibitishia kwamba atashiriki tamasha hilo.

"Kilahiro tutakuwa naye kwenye tamasha, na naamini kwamba
 mwaka huu tamasha hili litakuwa bora zaidi kutokana na
 kushirikisha waimbaji wengi wakali," alisema Msama.
 Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo la aina yake, baada ya
kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa
 Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9.
 Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia > mitaji wanawake wajane.
 Tamasha la Pasaka la mwaka huu litashirikisha waimbaji wa  nyimbo za Injili kutoka nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni  pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
 Congo, Afrika Kusini na Zambia.
 Akizungumza Dar es Salaam, Kilahiro alisema amepania kufanya mambo makubwa katika tamasha la mwaka huu, na atapanda  jukwaani kuimba 'live' na bendi yake ya Upendo Kilahiro.
 "Natoa mwito kwa mashabiki wangu wasiwe na wasiwasi,  watarajie kupata vitu vizuri na tofauti zaidi... watapata  vitu vinono kwa vile tamasha hili linazidi kuwa bora zaidi.
 "Sikukuu ya Pasaka ni upatanisho kutokana na kifo cha Yesu Kristo aliyefia msalabani na kufufuka siku ya tatu... tutaienzi sikukuu hiyo kwa nderemo," alisema Upendo.
 Mwanamuziki huyo anayeabudu katika Kanisa la BCIC lililoko Mbezi Beach, Dar es Salaam (Kwa Askofu Gamanywa), alisema amejiandaa vyema kukonga nyoyo za mashabiki wake na mbali na
 kufanya mazoezi, pia atafunga na kusali ili Mungu amfanyie miujiza.
 Aliwaomba mashabiki wamiminike kwa wingi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Aprili 8 na Jamhuri Aprili 9, kuona mambo  mazuri aliyowaandalia na kuongeza kuwa kwa vile anamtukuza
 Mungu aliyemtoa kwenye shida na majaribu mengi ya Shetani, anaamini atawapa kile wanachotaka kutoka kwakwe.
 Alisema anatarajia kuimba nyimbo mbalimbali zikiwemo zilizotamba za Zindonga (alioimba kwa Kizulu), Unajibu Maombi na Ni Salama Rohoni. Kilahiro hivi sasa anatamba na albamu yake mpya ya Ficho Langu aliyoirekodi nchini Canada.

Mauritius Beach team dreams of the Olympics

In few months, Mauritius Beach Volleyball pairing of Natasha Rigobert/ Elodie Li Youklo have become the most famous team in Africa not only because that cooperative team was one of 8 teams in Africa searching for the Olympic berth when they compete at the finals of the CAVB Continental Cup next June, but also because they were the gold medallists of the first ever Beach volleyball event to be held at the All Africa Games in Mozambique 2011.
In the history of All Africa Games that started in 1965 in Brazzaville, Congo and till the ninth edition in Alger 2007 only indoor volleyball competitions were organised till the organizing committee introduced beach volleyball in the programme at the tenth edition in Maputo, Mozambique 2011 where 12 African countries competed for the medals.
Mauritius pair Natasha Rigobert and Elodie Li Youklo had the honor to be the first ever gold medalists at this prestigious event after they defeated all the teams till they saw off South Africa in a thrilling finals which was televised all over the continent.
“We didn’t expect to get this honour when we started together playing beach as a team with my partner Elodie Li in 2008,” said Mauritius star Natasha Rigobert upon receiving the gold medal.
“When we defeated South Africa to get the first ever gold medal I didn’t realize that our dreams will be a reality very quickly like this,” remembered the Li the 3 years passed since she met Natasha for the first time.
“It was exciting that we met accidently together in Cannes, France in 2008 where we were attending a match together and we were both carrying the Mauritian flag in the tribune. I went directly to introduce myself to Natasha,” added Li.
“We had become friends before we know that both of us started to practice volleyball and we decided to make a team together and start the participation in the international beach volleyball competitions. As we are working together in France it was easy for both of us to practice regularly.”
In 2008 it was the first competition for Mauritius pairing to compete in Norway and it was the first also under their flag. They continued to participate in some international circuits together till the start of the CAVB Continental Cup which is the qualifying process for 2012 London Olympic Games.
“The continental Cup was a real implementation of beach volleyball activity in Africa and when we started playing in the sub zonal phase we felt proud to win the first competition in the African soil. It was in Namibia and at that time we decided to continue till we can get the African berth at the Olympics,” added Natasha and Li.
After losing the zonal phase final in Mozambique to the host country it was the first time that Natasha cried heavily with the tears dropping into the soil after the final match but she realized that she will come again to the same place the following month for the All Africa Games.
Natasha said to the journalists after the drawing of lots in Maputo that she is ready to cry another time in Mozambique. “This time I’m going to cry of joy after we top the podium with the gold medals,” commented Natasha.
“Now we have our eyes concentrating on the qualification to the Olympic Games when we play the final next June and at that time we will feel that we achieved something for our country. After we won the gold medal we received a call from the Mauritian Minister of Sport while we were sweating after the final and we promised him with the Olympic ticket.” Said Mauritius pair.
The Mauritian double wants to see Africa with a lot of beach volleyball courts because it is the future of the sport in the continent. “We need to see a lot of courts like this quality of Costa Do Sol Arena in Mozambique capital Maputo.”

Tuesday, February 21, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Februari 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam na kufanya uamuzi kwa ajenda mbalimbali ikiwemo Marekebisho ya Katiba za Wanachama wa TFF, na pia ushauri wa kisheria ulioombwa kwake na Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Uamuzi uliofanywa kwa wanachama wote 40 wa TFF ni ufuatao; wanachama wote wanatakiwa kufanya marekebisho kwenye katiba zao katika maeneo matatu kwa mujibu wa maelekezo ambayo TFF ilitoa mwaka jana.
Maeneo hayo ni sifa za wagombea uongozi ambapo kwenye kipengele cha elimu ni lazima iwe kuanzia kidato cha nne, kutopeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama za kawaida na kamati zao za uchaguzi kufanya kazi chini ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Hivyo hakuna mwanachama yeyote wa TFF anayeruhusiwa kufanya uchaguzi kwa sasa kama katiba yake ina upungufu au inakwenda kinyume na maelekezo kuhusu maeneo hayo matatu.
Kamati imetoa hadi Juni Mosi mwaka huu kwa wanachama ambao katiba zao zina upungufu katika maeneo hayo wawe wamefanya marekebisho ndiyo waendelee na uchaguzi kwa wale ambao muda wa uchaguzi umefika.
Ushauri wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ni kuwa katiba zote za wanachama ziwe na vitu hivyo vitatu.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji

Tamasha la Pasaka lafutwa CCM Kirumba

Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama amesema kuwa, tamasha hilo limepangwa kufanyika Aprili 9, katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Akizungumza jijini leo, Msama alisema kuwa, kamati imeamua kulihamishia tamasha hilo mkoani Dodoma badala ya Mwanza, baada ya kuridhika na maombi ya wadau wa muziki huo.

"Kamati kazi yake kubwa ni kupokea maoni kutoka kwa wadau na kuyafanyia kazi, wajumbe wameamua lifanyike mkoani Dodoma badala ya Mwanza," alisema.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa, awali tamasha hilo lilipangwa kufanyika mkoani Mwanza,
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Aprili 9, mwaka huu.

"Ni kitu cha kawaida kuhamisha sehemu moja kwenda sehemu nyingine, maamuzi ya kamati ni ya kuyaheshimu," alisema.

Mwaka jana, tamasha hilo lilifanyika katika mikoa mitatu, Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza.

Pia, Msama alisema kutokana na tamasha hilo kuwa la kimataifa, amewataka wafanyabiasha kujitokeza kudhamini tamasha hilo kubwa nchini.

Mpaka sasa, baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki, lakini kwa sasa wanaendelea na taratibu za kupata kibali cha kufanya kazi.

"Tayari baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje waliopelekewa mialiko, wamethibitisha kushiriki, kilichobaki ni kushughulishia vibali vyao," alisema.

"Bado tunapokea maoni kutoka kwa wadau wetu, tunaomba mzidi kututumia ili tuyafanyie kazi kabla ya tarehe ya tamasha hilo," alisema.

Tamasha la Pasaka mwaka huu litafanyika Aprili 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Aprili 9 litafanyika mkoani Dodoma.

Sunday, February 19, 2012

Niyonzima ataka wachezaji kujituma Cairo


KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amewataka wachezaji wenzake kujituma katika mchezo wao wa marudiano kwani Zamalek si timu ya kutishia maisha ya Yanga.
"Tunawamudu, soka yao si ya kutisha, nadhani wengi tulitishika na jina Zamalek ndiyo maana tukawa tunacheza kwa kutojiamini, lakini naamini mchezo wa marudiano utakuwa jibu tosha," alisema kiungo huyo aliyekuwa anajima uwanja mzima akitetea jahazi la Yanga lisiteketee katika mchezo huo.
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akijipumzisha.
Yanga na Zamalek zilikwaana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa timu hizo kufungana bao 1-1.
"Matokeo ya sare si mazuri sana kwetu ukizingatia tulikuwa tukicheza katika uwanja wa nyumbani na kupewa sapoti kubwa na mashabiki wetu," alisema Niyonzima.
"Ni hali ambayo tayari imetokea inatubidi kukubaliana nayo, tulitangulia kushinda lakini tukashindwa kulinda ushindi wetu kwa kutoa mwanya kwa wapinzani kusawazisha bao lile," aliongeza
"Hatutakiwi kukata tamaa hata kidogo kwa matokeo haya ya sare tuliyopata kwenye mchezo wa kwanza, nafikiri tujipange kwa wiki hizi mbili zijazo na kwenda kufanya maajabu kule mjini Cairo, Misri,"

Tamasha la Pasaka kufanyika Uwanja wa Taifa

Mandhari ya Uwanja wa Taifa
TAMASHA la Pasaka litakalofanyika Aprili 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam limepangwa kurindima kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuwa, kamati yake ilipokea maoni kutoka kwa wadau wa muziki huo na kuamua kufanyia tamasha hilo katika uwanja huo.

"Lengo letu ni kufanya tamasha letu katika sehemu kubwa ambayo itamwezesha kila mtu atakayekwenda kushuhudia, aridhike," alisema.

Mwaka jana, tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo wadau wa muziki huo walifurika na wengine kushindwa kuingia ndani.

Msama alisema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es Salaam, tamasha hilo litahamia mkoani Mwanza, katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Kutokana na tamasha hilo kuwa la kimataifa, Mwenyekiti huyo wa kamati ya maandalizi, aliwataka wafanyabiasha kujitokeza kudhamini tamasha hilo kubwa nchini.

Mpaka sasa, baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki, lakini kwa sasa wanaendelea na taratibu za kupata kibali cha kufanya kazi.

"Tayari baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje waliopelekewa mialiko, wamethibitisha kushiriki, kilichobaki ni kushughulishia vibali vyao," alisema.

"Bado tunapokea maoni kutoka kwa wadau wetu, tunaomba mzidi kututumia ili tuyafanyie kazi kabla ya tarehe ya tamasha hilo," alisema.

Tamasha la Pasaka mwaka huu litafanyika Aprili 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Aprili 9 litafanyika mkoani Mwanza.

Saturday, February 18, 2012

Simba droo ngoma, Yanga yabanwa Dar

Yanga imeshindwa kutumia uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Zamalek ya Misri katika mchezo mkali ulipigw akwenye Uwanja wa Taifa.
Yanga iliyokuwa imepania mchezo huo, imejiweka katika mazingira hatari, kwani Zamalek iliyovuliwa ubingwa na Simba 2003, itakuwa ikihitaji ushindi wa bao 1-0 au suluhu waweze kusonga mbele.
Ukiacha hayo ya yanga, Simba nayo imetoka sare ya 1-1 na Kiyovu ya Rwanda katika mchezo mwingine wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga kama ilivyo Simba, ilipata bao lake kupitia kwa Hamis Kiiza katika dakika ya 36 wakati lile la Simba lilifungwa na Mwinyi Kazimoto mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamirambo.
Zamalek ilisawaisha kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji wake matata Amr Zaki na kuiweza timu yake katika nafasi nzuri ya kusonga mbele wiki mbili zijazo.
Simba nayo inahitaji ushindi ama suluhu ya bila mabao iweze kuingia raundi ya kwanza kwani itakuwa na faida ya bao la ugenini.

Thursday, February 16, 2012

Wasanii wa kimataifa waalikwa Dar

WASANII wa nchi za nje wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la Pasaka ambalo limepangwa kufanyika Aprili 18 mwaka huu.
Mratibu wa tamasha hilo Alex Msama alisema wasanii hao ni kutoka Afrika ya Kusini, Zambia, Rwanda, Burundi na Kongo.
Alisema mbali na wasanii hao kutoka nje, pia tamasha hilo litasindikizwa na wasanii mbali mbali wa hapa nchini.
"Tumeshamalizana na wasanii wa nchi hizo, tupo kwenye hatua za mwisho za kumalizia taratibu za nchi kwa nchi kisha tutawaweka wazi,"alisema Msama
"Watu wategemee mambo makubwa kwenye tamasha la mwaka huu wasanii wakubwa wa nchi za nje na hapa nchini ndio watakaotumbuiza litakuwa tamasha la kimataifa, ni fursa nzuri pia kwa wasanii wa ndani kujenga mahusiano mazuri na wale wa nje.
Alisema mwaka huu tamasha hilo litafanyika sehemu mbili ambapo Dar es Salaam litafanyika Aprili 18 wakati Mwanza litafanyika Aprili 19.
Hivi karibuni, Msama alisema kuwa misaada yake itakuwa imewafikia watu milioni moja wakati tamasha hilo litakapotimiza miaka 20. Tamasha hilo litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu, litakuwa linatimiza miaka 12.
Alisema tamasha la mwaka huu limelenga kuwasaidia Watanzania wasiojiweza, walemavu, wajane na watoto yatima ambao wanasaidiwa fedha za ada na matumizi mbalimbali ya shule.

Kombe la Uefa lashika kasi

Lok'v Moscow v Athletic Bilbao 17:00
  • Ajax v Man Utd 18:00

  • AZ Alkmaar v Anderlecht 18:00

  • Lazio v Atl Madrid 18:00

  • Legia Warsaw v Sporting 18:00

  • Plzen v Schalke 04 18:00

  • SV Salzburg v Met'st Kharkiv 18:00

  • FC Porto v Man City 20:05

  • Hannover 96 v Club Brugge 20:05

  • Steaua Buch't v FC Twente 20:05

  • Stoke v Valencia 20:05

  • Trabzonspor v PSV Eindhoven 20:05
  • Miss Tanzania 2011, Salha Israel akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa nembo ya Miss Tanzania na Kampuni ya Bia Tanzania, TBL kupitia kinywaji chao cha Redd's kuwa ndiyo watakaodhamini mashindano ya mwaka huu. Mambo hayo yalikuwa Mlimani City juzi usiku.

    Simba watua Kigali kuwavaa Kiyovu

    Okwi, tegemeo SSC
    Wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba, wamewasili kwenye mji wa Kigali, Rwand tayari kwa mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Kiyovu Sports, mchezo utakaofanyika Jumamosi.
    Habari kutoka Kigali zinasema kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo.
    Wachezaji walioondoka ni makipa Juma Kaseja na Ali Mustapha 'Barthez'.
    Mabeki: Nassor Said 'Cholo', Juma Jabu, Juma Nyoso, Kelvin Yondan, Victor Costa na Obadia Mungusa.
    Viungo walioondoka ni Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na Patric Mafisango wakati washambuliaji ni Ramadhani Singano 'Messi', Edward Christopher, Salum Machaku na Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Emmanuel Okwi.
    Viongozi wa timu yumo Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange 'Kaburu', Katibu mkuu Evodius Mtawala, Fransis Silaya (Mjumbe wa kamati ya utendaji) Ibrahim Masoud, Milovan na msaidizi wake Amatre, Cosmas Kapinga (daktari) na James Kisaka ambae ni kocha wa makipa.

    POULSEN ATAJA 23 KUIVAA MSUMBIJI

    Add caption
    Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Jan Poulsen leo (Februari 16 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambalo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
    Kabla ya kuivaa Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi itakayochezwa Februari 29 mwaka huu, kikosi hicho kinatarajia kucheza mechi ya kirafiki Februari 23 mwaka huu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) itakayofanyika kwenye uwanja huo huo.
    Wachezaji wapya walioitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi hicho kitakachoingia kambini Februari 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni viungo Jonas Gerald (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
    Kikosi kamili kinaundwa na makipa Shabani Kado (Yanga), Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Juma Jabu (Simba), Stephen Mwasika (Yanga) na Kelvin Yondani (Simba).
    Viungo ni Jonas Gerard (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe (Simba), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Abdi Kassim (Azam).
    Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), John Bocco (Azam), Nizar Khalfan (Philadelphia Union, Marekani), Mrisho Ngasa (Azam), Ally Badru Ally (Canal Suez, Misri), Uhuru Selemani (Simba) na Nsa Job (Villa Squad).
    AFC NAYO YASHUKA DARAJA
    Timu ya AFC ya Arusha imeshindwa kutokea kwenye mechi ya Kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya 94 KJ iliyokuwa ichezwe jana (Februari 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
    Kwa mujibu wa Kanuni ya 21 ya FDL timu yoyote inayoshindwa kufika kituoni na kusababisha mchezo husika kutochezwa itashushwa daraja hadi Ligi ya Taifa na matokeo ya michezo yake yote itafutwa ili kutoa uwiano sahihi kwa timu zilizobaki kwenye mashindano.
    Si Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), msimamizi wa ligi hiyo Kituo cha Pwani wala Kamishna wa mechi hiyo Ramadhan Mahano waliokuwa na taarifa yoyote ya mapema juu ya AFC kushindwa kufika kituoni.
    AFC ambayo mbali ya kushushwa daraja inatakiwa kulipa faini ya sh. milioni moja kabla ya kucheza Ligi ya Taifa msimu ujao. Sh. 500,000 kati ya hizo zitakwenda kwa timu ya 94 KJ iliyoingia gharama za kujiandaa kwa mechi hiyo ambapo wapinzani wao hawakufika uwanjani.
    Kundi C la ligi hiyo sasa linabakiwa na timu nne baada ya Manyoni FC ya Singida nayo kushuka daraja kwa kushindwa kucheza mechi yake dhidi ya Polisi Tabora iliyokuwa ifanyike Februari 12 mwaka huu Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
    Timu zilizobaki katika kundi hilo ambalo baada ya mbili kujitoa hakuna itakayoshuka daraja ni 94 KJ ya Dar es Salaam, Polisi Tabora, Polisi Morogoro na Rhino FC ya Tabora.
    Powered by Sorecson : Creation de site internet
    Boniface Wambura
    Ofisa Habari
    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

    Wednesday, February 15, 2012

    Wafadhili, wadhamili waalikwa Tamasha la Pasaka

    <><>
    <>

    <><>

    Na Mwandishi Wetu
    KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, limefungua milango kwa wadau mbalimbali
    kudhamini tamasha hilo linalowakusanya watu wengi wa dini mbalimbali.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuwa, kamati yake itakuwa tayari kupokea udhamini kutoka kwa mtu ama kampuni yoyote bila ya kubagua.

    "Lengo la kuomba udhamini, ni kutaka kufanikisha tamasha hilo la kimataifa, kwani maandalizi yake ikiwemo kuwagharamia waimbaji ni kubwa sana," alisema.

    Msama alisema kuwa, tamasha hilo litapokea udhamini kutoka kwa dini zote, kwani lengo lake ni kumtukuza Mungu kupitia nyimbo za injili.

    Alisema pia wafanyabiadhara ambao watajitokeza kudhamini tamasha hilo, watapata baraka kubwa katika biashara zao na familia zao.

    Mpaka sasa, baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje ya nchi wameanza kuomba kushiriki, ambapo kamati ya tamasha hilo itakutana kupitia maombi yao na kuwatangaza.

    "Tayari baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na wale wa nje waliopelekewa mialiko wameanza kuthibitisha kushiriki, lakini kamati ndiyo itakayotangaza majina hayo," alisema.

    Msama alisema baada ya kupokea maombi kutoka kwa wadau wa tamasha hilo kutafuta sehemu kubwa ya wazi, kamati imeanza mchakato ambapo wakifanikiwa, wataitangaza.

    Mwenyekiti huyo wa tamasha alisema kuwa, tamasha la mwaka huu linatarajiwa kuwa la
    kimataifa zaidi kwa kuwashirikisha waimbaji kutoka nje ya nje.

    "Bado tunapokea maoni kutoka kwa wadau wetu, tunaomba mzidi kututumia ili tuyafanyie kazi kabla ya tarehe ya tamasha hilo," alisema.

    Tamasha la Pasaka mwaka huu litafanyika Aprili 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam,kabla ya kwenda mikoani.

    Monday, February 13, 2012

    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
    Februari 13, 2012
     
    14,150 WASHUHUDIA YANGA, RUVU SHOOTING
    Watazamaji 14,150 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Februari 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 47,554,000.
     
    Hata hivyo ni watazamaji saba tu waliokata tiketi za VIP A zilizokuwa zikiuzwa sh. 15,000. Viingilio vingine vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa na kiiingilio cha sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani kilichovutia watazamaji 12,853.
     
    Baada ya kuondoa gharama za awali za mechi hiyo namba 119 na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,254,000 kila timu ilipata sh. 8,583,000 wakati mgawo wa uwanja ulikuwa sh. 2,861,000.
     
    Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,144,400, TFF sh. 2,861,000, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,430,500, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 286,100 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 2,861,000.
     
    Gharama za awali za mechi ni nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna sh. 10,000, posho ya kujikimu kamishna sh. 40,000, posho ya kujikimu waamuzi sh. 120,000 na mwamuzi wa akiba sh. 30,000. Gharama za tiketi sh. 4,000,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
     
    Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 990,500 wakati DRFA ilipata sh. 849,000.
     
    Boniface Wambura
    Ofisa Habari
    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
     
     

    'Tevez akaribishwa tena Manchester City '

     
    Tevez
    MSHAMBULIAJI wa Man. City, Carlos Tevez ataanza mazoezi Jumanne Febr. 14  kwenye klabu hiyo baada ya jana kuwasili London kuendeela kuitumikia klabu yake hiyo.
    Tevez, 28, anatarajia kwenda kwenye sehemu ya mazoezi ya klabu hiyo iliyoko Carrington kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kuitumikia klabu yake.
    Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini amesema anamkaribisha na hana wasiwasi kwamba mchezaji huyo atashindwa kuitumikia klabu yake. Kila mmoja anafahamu kwamba Tevez ni mchezaji aliye juu na kwamba kila kitu kitakuwa kimemalizika kwa wakati” anasema kocha wa City, Roberto Mancini . "Sina tatizo na klabu wala mchezaji," anasema Mancini.
    Tevez anatarajiwa kupanda ndege kutoka Argentina kwenda England Jumanne. Na kocha anaamini klwamba kila kitu kitakuwa kimepatiwa utatuzi.

    Zambia coach dedicates Africa Cup of Nations win to crash dead

    Kocha wa Zambia, Herve akiwa juu ya wachezaji wake.
    Zambia coach Herve Renard dedicated his side's Africa Cup of Nations win to the victims of the plane crash that killed 18 members of the team in 1993.
    The Chipolopolo beat Ivory Coast 8-7 on penalties in Libreville, Gabon, to secure the trophy for the first time.
    "I told them if we got to the final we would play in Gabon where the plane crashed. There was a special significance in that," Renard said.
    "They found the strength. I don't know where," he added, fighting tears.
    Renard also praised the courage of Kalusha Bwalya, an iconic figure in Zambian football who would have been on the 1993 flight - which was taking the Zambia squad to a World Cup qualifier in Senegal when it crashed shortly after take-off from Libreville airport, killing all 30 people on board - but had made his own way there.
    "Kalusha was one of the best Zambian players of the last century," Renard said.
    "Then he was coach of the national team, now our [Football Association] president.
    "He knows how terrible this crash was for the nation.
    "I want to dedicate this title to him, he gave me my chance when nobody knew me."
    Football Association of Zambia (FAZ) president Bwalya, in turn, praised the French coach, and immediately looking ahead to the upcoming Nations Cup 2013 and World Cup 2014 qualifiers, said Renard "can stay as long as he wants".
    "I think that if he brings that discipline, that ambition that he has, as a coach, I think that he has made a statement for himself," Bwalya told BBC Sport.
    Stoppila Sunzu converted the winning spot-kick in the final for the jubilant Zambians, after Arsenal striker Gervinho missed for the Elephants following a goalless 120 minutes.
    The defeat saw Ivory Coast miss out on their second title, despite not conceding a goal from open play in the entire competition.
    Renard also described his side's unlikely triumph as an "enormous" achievement.
    "My players were magnificent," he said. "I know we're not the best but we have a strength and force that animated our team and made us African champions. They might make some tactical mistakes here and there but you can see the talent.
    "This is something enormous - something that appeared unrealisable before the competition began," added Renard, who managed Cambridge United briefly in 2004 , before spending two years in charge of French side AS Cherbourg

    Rest In Peace WHITNEY



    Sunday, February 12, 2012

    Yanga yaisogelea Simba kileleni

    Bao lililofungwa na Davis Mwape katika dakika ya 46, liliiwezesha Yanga kuibuka na ushindi huo katika mechi ya Ligi Kuu Bara, kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumapili jioni.
    Yanga imefikisha pointi 37 sawa na Simba na inaongoza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Azam ni ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.

    Zambia yaibeba Cosafa, Cecafa


    Raha ya ubingwa, Chipolopolo wakishangilia.
    Timu ya Taifa ya Zambia, 'Chipolopolo' imeubeba ukanda wa Kusini mwa Afrika na ule wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu, katika mchezo mkali wa fainali uliopigwa kwenye mji wa Libreville, Gabon.

    Zambia iliitoa Cote d'Ivoire kwa mikwaju ya penalti 8-7 na kuipa ubingwa wa michuano ya Afcon 2012 ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo.
    Timu hizo zilimaliza dakiak 120 zikiwa 0-0 katika mechi kali iliyopigwa Stade d'Angondjé mjini Libreville huku Didier Drogba akikosa penalti ya kipindi cha pili ambayo pengine ingewapa ushindi.
    Cote d'Ivoire wamecheza fainali nyingine huku wakiondoka wakiwa wamechanganyikiwa hasa kw akufungwa na Zambia waliokuwa wakishangilia huku wakiwaenzi wachezaji wenzao 18 waliokufa wakiitumikia timu hiyo waliokuwa mwaka 1993 kwenye pwani ya Gabon.
    Zambia nusura ipate bao dakika za mwanzoni kama Nathan Sinkala, angepiga shuti lenye akili lakini kipa Boubacar Barry alikuwa makini kuokoa hatari hiyo.
    Dakika ya 11, Joseph Musonda aliumia na nafasi yake ikajazwa na chipukizi, Nyambe Mulenga.
    Yaya Toure angeweza kuifungia timu yake bao baada ya kupata pasi kisigino ya Drogba.
    Emmanuel Mayuka nusura na yeye afanye vitu kama si uhodari wa kipa.

    Tamasha la Pasaka kufaidisha watu milioni 1

    Jukwaa likishambuliwa Diamond Jubilee mwaka jana
    Mwandishi Wetu

    ZAIDI ya watu milioni moja wenye matatizo anatarajia kufaidika na tamasha la Pasaka

    litakapotimiza miaka 20, tangu kuanzishwa kwake na kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini.

    Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tamasha hilo lililoanzishwa mwaka 2000, Alex

    Msama, alisema limelenga kuwasaidia Watanzania ilioni moja kwa kuwapatia misaada anuwai.

    Walengwa katika misaada hiyo ni wasiojiweza, walemavu, wajane na watoto yatima ambao

    wanasaidiwa fedha za ada na matumizi mbalimbali ya shule.

    Msama alisema lengo lake kubwa ni kwamba, tamasha hilo litakapotimiza miaka 20 tangu

    kuanzishwa kwake, Watanzania wasiopungua milioni moja wawe wamenufaika nalo, ambapo

    mwaka huu ni la kimataifa.

    "Tusiitegemee Serikali kwa kila kitu, haiwezi kumsaidia kila mtu, vitu vingine tunatakiwa

    tufanye wenyewe kwa ajili ya kusaidia wenzetu upitia vyanzo mbalimbali kama hili tamasha,"

    alisema.

    Msama alisema maandalizi ya tamasha la mwaka uu yanaendelea vizuri, ambapo tayari

    wamepatiwa kibali na litafanyika sehemu ya wazi ili liweze kushuhudiwa na wadau wengi wa muziki

    huo.

    Licha ya maandalizi kuanza mapema, Msama alisema tamasha hilo la kimataifa litawahusisha

    waimbaji wa muziki huo wa kimataifa ambao watatangazwa hapo baadaye.

    Msama aliwataka waimbaji wazawa kuhakikisha mwaka huu, wanatumia vyombo vya muziki moja

    kwa moja, kwani suala la CD linaweza lisitumiwe. "Wasanii mwaka huu watakuwa wengi zaidi ya

    mwaka jana, nawaomba waimbaji wa nyumbani wasitumie CD, kama ilivyokuwa mwaka jana nusu

    nzima ya wasanii walitumia," alisema

    Mbali ya mandalizi hayo kuendelea, wamekuwa na wakati mgumu kuamua tamasha hilo lifanyike
    mkoa gani kwa sababu mikoa kama Mbeya,

    Kilimanjaro, Mwanza, Arusha na Morogoro imeomba baada ya kufamnyika Dar es Salaam

    Aprili 8, mwaka huu, lihamie huko.

    "Hatujajua litaelekea wapi baada ya Dar es Salaam, ila tuko katika mazungumzo kuona lifanyike mkoa

    gani kati ya mikoa hii iliyoomba... baada ya siku chache tutatoa taarifa rasmi litaendelea wapi,"

    alisema.

    Saturday, February 11, 2012

    Eee Kidedea....eeee kidedeaaaa..

    Simba 'yailambisha koni' Azam


    Simba ya Dar es Salaam, imeichapa Azam FC mabao 2-0 katika mechi kali ya Ligi Kuu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Mechi hiyo iliyokuwa na kila aina ya mashamsham, ilianza kwa Azam kulishambulia lango la Simba ambao wamerudi kileleni kwa kufikisha pointi 37 huku Yanga ikiendelea na nafasi yake ya pili kwa kuwa na pointi 34 wakati Azam inabaki na pointi zake 32.
    Mchezo wa leo ulikuwa wa ubabe, kila timu ilikuwa ikicheza kitemi, lakini Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 10, lakini mwamuzi alilikataa kwa madai mfungaji alikuwa ameotea.
    Dakika ya 30, Emmanuel Okwi aliwanyanyua mashabiki wa Simba kwa kufunga bao safi na kumwacha kipa wa Azam, Mwadin Ally akiwa hana la kufanya.
    Okwi alipachika bao la pili dakika 70 baada ya kutanguliziwa mpira wa kichwa na Felix Sunzu ambaye hata hata hivyo, baadaye aliumia na kutoka.
    Kocha wa Azam, Stewart Hall aliwalaumu wachezaji wake kutokuwa makini na mchezo, lakini akasema ndivyo soka ilivyo wakati mwenzake wa Simba aliwapongeza wachezaji wake kwa kazi nzuri.
    Mbali na matokeo hayo, Toto African ilitoka suluhu na Moro United wakati Villa Squad iliifumua Polisi Dodoma kwa kuichapa mabao 2-1.
    Mechi nyingine, Coastal Union iliifunga African Lyon bao 1-0 kabla ya JKT Olchoro kuwafunga wenzao wa Ruvu bao 1-0.

    Matokeo ya Ligi Kuu England leo



    Man Utd 2 - 1 Liverpool
    Blackburn 3 - 2 QPR 
  • Bolton 1 - 2 Wigan 
  • Everton 2 - 0 Chelsea 
  • Fulham 2 - 1 Stoke 
  • Sunderland 1 - 2 Arsenal 
  • Swansea 2 - 3 Norwich 
  • Friday, February 10, 2012

    Tamasha la Pasaka lapata kibali

    Wednesday, February 8, 2012

    Dewji awapa Chipolopolo sh. mil. 22


    AZIM DEWJI

    Tuesday, February 7, 2012

    Wadau waipa shavu Basata

    BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limepongezwa na wadau wa Sanaa kwa juhudi zake katika kusimamia na kuratibu matukio mbalimbali ya Sanaa hapa nchini na kuyafanya kudumu.
    Pongezi hizo zimetolewa wiki hii na wadau wa Sanaa wakati wakichangia mjadala uliohusu miaka mitano ya shindano la miss utalii na sanaa ya urembo nchini kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA uliopo Ilala, Sharif Shamba.
    Akizungumza wakati akieleza historia za shindano hilo, Rais wa Miss Utalii, Gideon Chipungahelo alisema kuwa, BASATA imekuwa bega kwa bega na shindano hilo katika kuhakikisha miongozo na kanuni mbalimbali za kuendesha mashindano zinafuatwa na kusisitiza kuwa, hiyo ndiyo sababu ya shindano hilo kuweza kupata baadhi ya mafanikio ya ndani na nje ya nchi.
    “Naishukuru Serikali na BASATA, kila mara wamekuwa wakitoa maelekezo na miongozo ambayo imelifanya shindano hili kufikia mafanikio haya ingawa kumekuwa na changamoto kadhaa hasa za kukosa wadhamini” alisistiza Chipungahelo.
    Aliongeza kuwa, BASATA imekuwa mara kwa mara ikikutana na kamati ya miss utalii na kuipa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini na wadau wa sanaa ya urembo ambao wamekuwa wakitoa michango ya kuliboresha shindano hilo.

    Monday, February 6, 2012

    TOC wanoa makocha wa ngumi

    Mwandishi Wetu, Kibaha
    KAMATI ya Olimpiki Tanzania, TOC, imelitaka Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania, BFT, kuueneza mchezo huo katika mikoa mbalimbali kwani kufanya hivyo kutainua mchezo huo.
    Hayo yalisemwa na Katibu wa TOC, Filbert Bayi wakati akifungua mafunzo ya makocha ngumi za ridhaa, yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule za Filbert Bayi, Kibaha mkoani Pwani.
    Mafunzo hayo yameandaliwa na TOC kwa kushirikiana na Kamati ya Misaada ya Olimpiki, Olympic Solidarity, OS, ambayo ina kazi ya kuendesha mafunzo na misaada mbalimbali kuhusiana na michezo mbalimbali.
    Bayi alisema kuwa BFT wana kazi ya ziada kuinua na kuueneza mchezo huo na kuachana na dhana ya kuutegemea mkoa wa Dar es Salaam ama mashindano kufanyika mkoani humo pekee.
    "Bado BFT wana kazi ngumu, ngumi zimekuwa zikipiganwa mkoa wa Dar es Salaam na hasa katika majeshi...yakifanyika mashindano, ni mikoa michache inashiriki na kutoa nafasi ndogo ya ushiriki.
    "Naomba kuchukua nafasi hii kuwashauri viongozi wa BFT kuueneza mchezo huu mikoani na mikoani ndiko kwenye wachezaji na vipaji vingi kuliko kuliko kutegemea klabu zilizoko mjini pekee," alisema.
    Kwa muda mrefu, Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, IOC, imekuwa ikitoa mafunzo ya utaalam kwa makocha mbalimbali ikiwemo wa ngum kwa kuwa mchezo huo ni miongoni mwa michezo inayoshindaniwa katika Michezo ya Olimpiki.
    "TOC na IOC zinataka kuona ngumi zinapiga hatua na ndiyo maana zinatoa mafunzo kwa kuleta wataalam...ni gharama kuleta makocha lakini wanapopatikana wataalamu, tutumie mafunzo kuwapa walimu wenye taaluma na watutengenezee vijana.

    Mabondia wa Tanzania kuweka kambi London

    Mwandishi Wetu
    MABONDIA wa Tanzania watakaofuzu Michezo ya Olimpiki baada ya mapambano ya mchujo yatakayofanyika kwenye mji wa Cassablanca nchini Morocco, wataweka kambi ya miezi mitatu London kabla ya michezo hiyo.
    Katibu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania, Makore Mashaga alisema jana mjini Kibaha, Pwani kuwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, OIC, imetoa ofa hiyo kwa mabondia wa Tanzania.
    Mashindano ya mchujo ya mabondia watakaoshuiriki Michezo ya Olimpiki, itafanyika baadaye Aprili.
    "Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki wametupa ofa hiyo, sasa kinachosubiriwa ni kupatikana na kwa mabondia hao.
    Mashaga aliwatoa wasiwasi Watanzania kwa kusema kuwa mwaka huu Tanzania itapitisha mabondia wengi katika michezo hiyo kwa kuwa wana vipaji na morali wa hali ya juu.
    Hata hivyo, mbali na hali hiyo, aliwataka wadau mbalimbali na zaidi serikali kusaidia kwa kiasi kikubwa maandalizi kwani uhakika wa kupata medali mwaka huu ni mkubwa katika historia ya ngumi Tanzania.
    Wakati huo huo, Mashaga amesema kuwa kambi za mabondia zinaendelea vizuri ikiwemo ya Mgulani inayoongozwa na Ben Mwangata, Mazimbo Ally, Fatuma Milanzi na Rogata Damiani.
    Kambi ya Mwenge iko chini ya Timoth Kingu, David Yombayomba na Hilal Kangoma na ile ya Magereza inaongozwa na Remmy Ngabo, Mussa Maisori, Hamis Shaaban na Kameda Anthony.
    Alisema kambi ya Uwanja wa Taifa inaongozwa na karoli Akabinjuka, Said Omari na Emmanuel Imma.
    Mashaga alisema mabondia 50 waliopatikana watachujwa hadi 20 ili kupata timu ya taifa na baadaye 10 watakaokwenda Cassablanca.