Mratibu wa tamasha hilo Alex Msama alisema wasanii hao ni kutoka Afrika ya Kusini, Zambia, Rwanda, Burundi na Kongo.
Alisema mbali na wasanii hao kutoka nje, pia tamasha hilo litasindikizwa na wasanii mbali mbali wa hapa nchini.
"Tumeshamalizana na wasanii wa nchi hizo, tupo kwenye hatua za mwisho za kumalizia taratibu za nchi kwa nchi kisha tutawaweka wazi,"alisema Msama

Alisema mwaka huu tamasha hilo litafanyika sehemu mbili ambapo Dar es Salaam litafanyika Aprili 18 wakati Mwanza litafanyika Aprili 19.
Hivi karibuni, Msama alisema kuwa misaada yake itakuwa imewafikia watu milioni moja wakati tamasha hilo litakapotimiza miaka 20. Tamasha hilo litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu, litakuwa linatimiza miaka 12.
Alisema tamasha la mwaka huu limelenga kuwasaidia Watanzania wasiojiweza, walemavu, wajane na watoto yatima ambao wanasaidiwa fedha za ada na matumizi mbalimbali ya shule.
No comments:
Post a Comment