Jukwaa likishambuliwa Diamond Jubilee mwaka jana |
ZAIDI ya watu milioni moja wenye matatizo anatarajia kufaidika na tamasha la Pasaka
litakapotimiza miaka 20, tangu kuanzishwa kwake na kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tamasha hilo lililoanzishwa mwaka 2000, Alex
Msama, alisema limelenga kuwasaidia Watanzania ilioni moja kwa kuwapatia misaada anuwai.
Walengwa katika misaada hiyo ni wasiojiweza, walemavu, wajane na watoto yatima ambao
wanasaidiwa fedha za ada na matumizi mbalimbali ya shule.
Msama alisema lengo lake kubwa ni kwamba, tamasha hilo litakapotimiza miaka 20 tangu
kuanzishwa kwake, Watanzania wasiopungua milioni moja wawe wamenufaika nalo, ambapo
mwaka huu ni la kimataifa.
"Tusiitegemee Serikali kwa kila kitu, haiwezi kumsaidia kila mtu, vitu vingine tunatakiwa
tufanye wenyewe kwa ajili ya kusaidia wenzetu upitia vyanzo mbalimbali kama hili tamasha,"
alisema.
Msama alisema maandalizi ya tamasha la mwaka uu yanaendelea vizuri, ambapo tayari
wamepatiwa kibali na litafanyika sehemu ya wazi ili liweze kushuhudiwa na wadau wengi wa muziki
huo.
Licha ya maandalizi kuanza mapema, Msama alisema tamasha hilo la kimataifa litawahusisha
waimbaji wa muziki huo wa kimataifa ambao watatangazwa hapo baadaye.
Msama aliwataka waimbaji wazawa kuhakikisha mwaka huu, wanatumia vyombo vya muziki moja
kwa moja, kwani suala la CD linaweza lisitumiwe. "Wasanii mwaka huu watakuwa wengi zaidi ya
mwaka jana, nawaomba waimbaji wa nyumbani wasitumie CD, kama ilivyokuwa mwaka jana nusu
nzima ya wasanii walitumia," alisema
Mbali ya mandalizi hayo kuendelea, wamekuwa na wakati mgumu kuamua tamasha hilo lifanyike
mkoa gani kwa sababu mikoa kama Mbeya,
Kilimanjaro, Mwanza, Arusha na Morogoro imeomba baada ya kufamnyika Dar es Salaam
Aprili 8, mwaka huu, lihamie huko.
"Hatujajua litaelekea wapi baada ya Dar es Salaam, ila tuko katika mazungumzo kuona lifanyike mkoa
gani kati ya mikoa hii iliyoomba... baada ya siku chache tutatoa taarifa rasmi litaendelea wapi,"
alisema.
No comments:
Post a Comment