Sunday, February 19, 2012

Niyonzima ataka wachezaji kujituma Cairo


KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amewataka wachezaji wenzake kujituma katika mchezo wao wa marudiano kwani Zamalek si timu ya kutishia maisha ya Yanga.
"Tunawamudu, soka yao si ya kutisha, nadhani wengi tulitishika na jina Zamalek ndiyo maana tukawa tunacheza kwa kutojiamini, lakini naamini mchezo wa marudiano utakuwa jibu tosha," alisema kiungo huyo aliyekuwa anajima uwanja mzima akitetea jahazi la Yanga lisiteketee katika mchezo huo.
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akijipumzisha.
Yanga na Zamalek zilikwaana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa timu hizo kufungana bao 1-1.
"Matokeo ya sare si mazuri sana kwetu ukizingatia tulikuwa tukicheza katika uwanja wa nyumbani na kupewa sapoti kubwa na mashabiki wetu," alisema Niyonzima.
"Ni hali ambayo tayari imetokea inatubidi kukubaliana nayo, tulitangulia kushinda lakini tukashindwa kulinda ushindi wetu kwa kutoa mwanya kwa wapinzani kusawazisha bao lile," aliongeza
"Hatutakiwi kukata tamaa hata kidogo kwa matokeo haya ya sare tuliyopata kwenye mchezo wa kwanza, nafikiri tujipange kwa wiki hizi mbili zijazo na kwenda kufanya maajabu kule mjini Cairo, Misri,"

No comments:

Post a Comment