![]() |
Raha ya ubingwa, Chipolopolo wakishangilia. |
Timu ya Taifa ya Zambia, 'Chipolopolo' imeubeba ukanda wa Kusini mwa Afrika na ule wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu, katika mchezo mkali wa fainali uliopigwa kwenye mji wa Libreville, Gabon.
Zambia iliitoa Cote d'Ivoire kwa mikwaju ya penalti 8-7 na kuipa ubingwa wa michuano ya Afcon 2012 ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo.
Timu hizo zilimaliza dakiak 120 zikiwa 0-0 katika mechi kali iliyopigwa Stade d'Angondjé mjini Libreville huku Didier Drogba akikosa penalti ya kipindi cha pili ambayo pengine ingewapa ushindi.
Cote d'Ivoire wamecheza fainali nyingine huku wakiondoka wakiwa wamechanganyikiwa hasa kw akufungwa na Zambia waliokuwa wakishangilia huku wakiwaenzi wachezaji wenzao 18 waliokufa wakiitumikia timu hiyo waliokuwa mwaka 1993 kwenye pwani ya Gabon.
Zambia nusura ipate bao dakika za mwanzoni kama Nathan Sinkala, angepiga shuti lenye akili lakini kipa Boubacar Barry alikuwa makini kuokoa hatari hiyo.
Dakika ya 11, Joseph Musonda aliumia na nafasi yake ikajazwa na chipukizi, Nyambe Mulenga.
Yaya Toure angeweza kuifungia timu yake bao baada ya kupata pasi kisigino ya Drogba.
Emmanuel Mayuka nusura na yeye afanye vitu kama si uhodari wa kipa.
No comments:
Post a Comment