![]() |
Tevez |
MSHAMBULIAJI wa Man. City, Carlos Tevez ataanza mazoezi Jumanne Febr. 14 kwenye klabu hiyo baada ya jana kuwasili London kuendeela kuitumikia klabu yake hiyo.
Tevez, 28, anatarajia kwenda kwenye sehemu ya mazoezi ya klabu hiyo iliyoko Carrington kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kuitumikia klabu yake.
Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini amesema anamkaribisha na hana wasiwasi kwamba mchezaji huyo atashindwa kuitumikia klabu yake. “Kila mmoja anafahamu kwamba Tevez ni mchezaji aliye juu na kwamba kila kitu kitakuwa kimemalizika kwa wakati” anasema kocha wa City, Roberto Mancini . "Sina tatizo na klabu wala mchezaji," anasema Mancini.
Tevez anatarajiwa kupanda ndege kutoka Argentina kwenda England Jumanne. Na kocha anaamini klwamba kila kitu kitakuwa kimepatiwa utatuzi.
No comments:
Post a Comment