![]() |
Mandhari ya Uwanja wa Taifa |
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuwa, kamati yake ilipokea maoni kutoka kwa wadau wa muziki huo na kuamua kufanyia tamasha hilo katika uwanja huo.
"Lengo letu ni kufanya tamasha letu katika sehemu kubwa ambayo itamwezesha kila mtu atakayekwenda kushuhudia, aridhike," alisema.
Mwaka jana, tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo wadau wa muziki huo walifurika na wengine kushindwa kuingia ndani.
Msama alisema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es Salaam, tamasha hilo litahamia mkoani Mwanza, katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Kutokana na tamasha hilo kuwa la kimataifa, Mwenyekiti huyo wa kamati ya maandalizi, aliwataka wafanyabiasha kujitokeza kudhamini tamasha hilo kubwa nchini.
Mpaka sasa, baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki, lakini kwa sasa wanaendelea na taratibu za kupata kibali cha kufanya kazi.
"Tayari baadhi ya waimbaji nyota wa ndani na nje waliopelekewa mialiko, wamethibitisha kushiriki, kilichobaki ni kushughulishia vibali vyao," alisema.
"Bado tunapokea maoni kutoka kwa wadau wetu, tunaomba mzidi kututumia ili tuyafanyie kazi kabla ya tarehe ya tamasha hilo," alisema.
Tamasha la Pasaka mwaka huu litafanyika Aprili 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Aprili 9 litafanyika mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment