Monday, February 6, 2012

Mabondia wa Tanzania kuweka kambi London

Mwandishi Wetu
MABONDIA wa Tanzania watakaofuzu Michezo ya Olimpiki baada ya mapambano ya mchujo yatakayofanyika kwenye mji wa Cassablanca nchini Morocco, wataweka kambi ya miezi mitatu London kabla ya michezo hiyo.
Katibu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania, Makore Mashaga alisema jana mjini Kibaha, Pwani kuwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, OIC, imetoa ofa hiyo kwa mabondia wa Tanzania.
Mashindano ya mchujo ya mabondia watakaoshuiriki Michezo ya Olimpiki, itafanyika baadaye Aprili.
"Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki wametupa ofa hiyo, sasa kinachosubiriwa ni kupatikana na kwa mabondia hao.
Mashaga aliwatoa wasiwasi Watanzania kwa kusema kuwa mwaka huu Tanzania itapitisha mabondia wengi katika michezo hiyo kwa kuwa wana vipaji na morali wa hali ya juu.
Hata hivyo, mbali na hali hiyo, aliwataka wadau mbalimbali na zaidi serikali kusaidia kwa kiasi kikubwa maandalizi kwani uhakika wa kupata medali mwaka huu ni mkubwa katika historia ya ngumi Tanzania.
Wakati huo huo, Mashaga amesema kuwa kambi za mabondia zinaendelea vizuri ikiwemo ya Mgulani inayoongozwa na Ben Mwangata, Mazimbo Ally, Fatuma Milanzi na Rogata Damiani.
Kambi ya Mwenge iko chini ya Timoth Kingu, David Yombayomba na Hilal Kangoma na ile ya Magereza inaongozwa na Remmy Ngabo, Mussa Maisori, Hamis Shaaban na Kameda Anthony.
Alisema kambi ya Uwanja wa Taifa inaongozwa na karoli Akabinjuka, Said Omari na Emmanuel Imma.
Mashaga alisema mabondia 50 waliopatikana watachujwa hadi 20 ili kupata timu ya taifa na baadaye 10 watakaokwenda Cassablanca.

No comments:

Post a Comment